MAMLAKA YA MAPATO NCHINI TANZANIA .( TRA) IMEADHIMISHA SIKU YA FORODHA DUNIANI

 


Na. Sheila Ahmadi


Mamlaka ya mapato  nchini Tanzania imeadhimisha siku ya Forodha duniani ikiwa na lengo la kuweza kuhamasisha. Ulipaji wa Jodi kutoka kwenye  makampuni mablimbali na kuweza kulipa kodi  kwa wakati kupitia biashara mbalimbali 


Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam Kaimu Kamishna wa Forodha, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Hassan Juma amesema Maadhimisho hayo yameweza kufanyika   Dar es Salaam kutokana na  uwepo wa wadau wengi wa forodha na kuwatambua baadhi ya wadau ambao wanafanya kazi kwenye Taasisi mbalimbli za kiserikali na binafsi.


Kila. Inapofika. Januari 26 kila mwaka Idara ya forodha Tanzania inaadhimisha kwa  mwanachama wote ambao wanafanya kazi  kutoka kwenye  Mamlaka hiyo  ya Forodha Duniani  hivyo kupitia TRA inaenda kuhamasisha ulipaji wa mapato nchini na kuendeleza uchumi wa nchi kutokana na  kodi ambazo zinatolewa.



"lengo la maadhimisho hayo   ni kwenda  kutoa ujumbe   kwa Umma juu ya shughuli. Ambazo  zinazofanywa na Wadau wa Forodha nchini hivyo  sisi  Tunatambua umuhimu wa  wadau  hao ambao wameweza kushiriki   katika kufanya shughuli  hii ya  forodha.


Aidha kamishina juma. Amesema kuwa mwaka huu Mamlaka ya Forodha Ulimwenguni (WCO), imetoa kauli mbiu ya Kutambua na Kuthamini juhudi na michango ya wadau mbalimbali katika kushirikiana   na Wakala wa forodha nchini  hivyo tumejipanga vyema katika kuhakikisha,na  kutimiza majukumu ya kiforodha " Amesema.Kamishina Juma"


Hata hivyo  amesema  kuwa watawatambua wadau wa Forodha ambao wanafanyanao kazi ambao wanaweza kuwa Serikali, Makampuni binafsi, na  Umma  ambapo wataweka mazingira wezeshi ambayo yataenda kuwasaidia kutekeleza majukumu ya Kiforodha ambayo ni Kukusanya Mapato, Kusimamia mipaka na kuilinda jamii.


Vilevile   utambuzi huo unatokana na majukumu ya kukagua bidhaa zinapoingia nchini ambazo haziruhusiwi lakini pia bidhaa zinazoingia nchini mpaka kupata vibali au ruhusa.


Forodha ina majukumu  ya Mamlaka kubwa hapa nchini  na ulimwenguni kote katika.kuweza  kusimamia, kukusanya mapato ya Serikali na kulinda jamii ya watumiaji wa bidhaa mbalimbali.



Ukuaji  wa  Teknolojia nchini umeweza  kusaidia mambo mengi yakiwemo ulinzi na usalama na sio kama  zamani ilikuwa  ni. kuwasilisha nyaraka kwa mkono kwa sasa hicho kitu ni historia hivyo zinaenda.  Kutumwa kwa mtandao, ambapo unapata tathmini ya kila kitu  pamoja na Kulipia.


Naye. Kamanda. Wa polisi kanda ya dar es salaam Jumanne. Murilo amesema ukaguzi wa Mizigo  unatumia kifaa maalumu cha ukaguzi ambacho hufanya kazi kwa muda mfupi zaidi ambapo zamani ilichukua muda mwingi na rasilimali watu huku jeshi. La polisi likiwa na jukumu ya kulinda Amani  ili kuzuia ubadhirifu wa Mali za watu.


Tunawakumbusha wananchi wafahamu thamani ya ulipaji wa kodi kwani nimekuwa nikifatilia kwa karibu mno wantazania wanapenda kutumia vitu vizuri  ikiwemo huduma bora na vyenye thamani hivyo ulipaji wa kodi ni jukumu la kila Mwananchi kwaio wito wangu kwa wananchi ni kulipa kodi kwani tunaenda kujenga nchi .


Mchango wa jeshi la forodha katika maadhimisho hayo ni kuweza kuimarisha usalama wa nchi kwani tunataka wananchi wafanye vizuri biashara Zak na wawe katika mazingira wezeshi na pindi wapatapo faida waweze kulipa kodi. "Amesema. kamanda murilo


Post a Comment

0 Comments