Na sheila Ahmadi
Akizungumza mara baada ya kutembelea daraja lililopo kunduchi Mtongani Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema kuwa madaraja ambayo yamedhurika. na janga la mvua serikali inaenda kuleta mawasikiano ya haraka kwa madaraja yote ambayo yameharibika na kuwataka Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD), kuhakikisha kuwa wanakuja na mpango madhubuti wa muda mrefu wa kutengeneza njia sahihi ya maji.
Aidha kasekenya amewataka wahandisi mkoani humo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye kingo za madaraja hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha nchini kwani mvua hizo zinaenda kupelekea changamoto kwa wakazi wa maeneo hayo.
Kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa wakala wa barabara TANROADS wanaendelea kukagua miundombinu katika maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua hizo ikiwamo Jangwani, daraja la Kunduchi na mengineyo
"TANROAD waanze kufanya ukaguzi haraka iwezekanavyo ili waweze kuweka alama za tahadhari kwenye barabara ili ziweze kwenda kuwasaidia wananchi pindi athari zinapotokea.
Nyinyi TANROAD ndio wenye kujua changamoto na viashiria vya hatari, sasa ni vyema muwe mnafanya ukaguzi ili mtoe tahadhari ya haraka kwa wananchi ili kwenda kuepuka madhara mbalimbali yanayojitokeza kama haya ambayo yameweza kujitokeza,” amesema Mhandisi Kasekenya.
Natoa rai kwa wakazi wa maeneo yote jijini dar es saalam kuchukua tahadhari wanapopita katika maeneo ya madaraja, wakiona maji mengi na sehemu ya ardhi haionekani wasipite.
Niipongeze sana serikali ya awamu ya sita ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake pindi Mamlaka ya Hali ya Hewa(TMA) ilipotangaza uwepo wa mvua hizi kubwa alitoa maelekezo kwa wizara zote kujiandaa na kukabiliana na changamoto zozote zitakazotokea ndio maana unaona changamoto hii ilipotokea wenzetu TANROAD makao makuu na mkoa wameshughulikia hizi changamoto kwa haraka,”amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni, Saad Mtambule ameipongeza TANROAD wa mkoa huo na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa jitihada kubwa waliyoofanya za kurudisha huduma ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo Mhandisi Suzana Lukasi amesema mvua imeharibu miundombinu ya madaraja na barabara lakini juhudi kubwa imefanyika ya kuhakikisha miundombinu hiyo inarejeshwa kwa wakati.
“Mvua hizi zilizonyesha zimesababisha uharibifu mkubwa lakini tumejitahidi kuhakikisha miundombinu hiyo tunairekebisha na sasa tumefungua njia zinapitika huku ukarabati mwingine.



0 Comments