TPA YATIMIZA MALENGO MADHUBUTI YA UTOAJI WA HUDUMA WEZESHI YA MAKASHA BANDARINI MWEZI JULAI HADI DISEMBA 2023





Na  Sheila   Ahmadi 


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeweka  lengo la uhudumiaji wa makasha kwa asilimia 2.8 katika kipindi cha Julai hadi Desemba , 2023.


Akizungumza  na Wanahabari  na wahariri Jijini Dar es Salaam    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Plasduce Mbossa wakati akitoa ufafanuzi kuhusu utendaji na uendeshaji wa Bandari nchini kwa waandishi wa Habari.


Mkurugenzi    mbosa  amesema  kiwango cha   meli na shehena kwenye  kipindi cha mwezi Julai hadi Di semba 2023 ni matokeo ya maboresho ya Bandari ambapo yaliweza  kufanywa  na  Serikali    ya awamu ya sita  huku  kupitia wizara  ya mamlaka ya bandari  TPA   pamoja na kuimarika kwa Sera za uwekezaji nchini.


Kutokana na  uboreshaji  wa mazingira wezeshi kuwa kupitia Sera ya Diplomasia ya Uchumi inayotekelezwa na serikali  ya jamhuri ya muungano wa Tanzania  imeweza kuchangia  ongezeko la Meli  kupitia Bandari ya Dar es Salaam na kuendelea kuboreshwa kwa Bandari nyingine nchini na kuvutia wawekezaji  katika kuendeleza uchumi.


Aidha  amesema matokeo hayo ni jitihada  ambazo  zimefanywa  na  serikali katika kuimarisha uchumi wa nchi hivyo amepongeza kwa mikakati thabiti ya kukuza uchumi na Sera madhubuti za Uwekezaji nchini.


Vilevile   amesema changamoto zilizopo katika mamlaka hiyo ya bandari   ikiwemo muda wa upakuaji wa meli na udogo wa eneo  hivyo kama wafanyakazi   wameanza  kuzifanyia kazi Kwa haraka  ili   kuongeza magati mengine 9 tisa


Suala  la  Bandari ya Bagamoyo amesema mradi huo unaendelea  hivyo kwa sasa wanatangaza zabuni kwa mujibu wa sheria.


Naye   mtendaji kutoka   Bandari ya Dar es Salaam baada ya kuingia kwa Mwekezaji mpya mwaka huu kupitia   kampuni ya DP-World wanaendelea na makabidhiano  ya kisheria huku wafanyakazi wataamua kuendelea kufanya kazi TPA au kuhamia DP-World.

Post a Comment

0 Comments