WIZARA YA MAMBO YA NJE LIMEFANYA KONGAMANO LA MAPENDEKEZO YA MAREKEBISHO YA SERA MPYA .


Na   Sheila  Ahmadi


Wizara  ya mambo ya  nje  na ushirikiano wa Afrika mashariki   imefanya kongamano na wadau mbalimbali jijini  dar es  aalaam   ili  kuweza kupendekeza  na kurekebisha  sera  mpya ya wizara hiyo  katika kuweka maendeleo na vielelezo madhubuti  hususani  sera mpya katika wizara hiyo.




Hayo  yamesemwa  na Waziri  wa  mambo ya nje  na ushirikiano wa afrika  mashariki  Mh  January  makamba ambapo  amesema kuwa katika kujenga sera mpya lazima tuwajibike katika lengo husika na kwenda kuleta  Chachu kwa Maendeleo ya nchi.


Aidha  Waziri  makamba amesema  kuwa katika kukusanya maoni hayo ya wadau  ni kuhusisha marekebisho ya sera  mpya kutoka kwenye wizara ya mambo ya ndani hivyo  wadau ambao mmeshiriki kwenye kongamano hili ni vyema kwenda kuleta sera nzuri ambayo itakuwa inatumika kwa mambo mbalimbali.


"Amesema kama nchi  inafanya mambo yaliyo sahihi lazima iweze  kujikita katika  ushawishi ikiwemo nchi ya Tanzania  imejikita zaidi katika kufanya  mambo ya ushawishi  ambayo yataenda kulifanya nchi kuingia katika ubora wa hali ya juu "Amesema  Waziri  Mbarawa".


Waziri   makamba    amesema  katika kufanyiwa  marekebisho  ya sera  hiyo  wizara  hiyo  imelazimika  katika kufanya  mabadiliko mbalimbali ambayo yametokea duniani  kwa wakati huu hivyo  imelazimu Nchi  ya Tanzania  katika kuendesha  kwa mujibu wa  mabadiliko  hayo.


Katika hatua nyingine amesema katika mabadiliko hayo yakiwemo  na tabia ya nchi   kuibua Taasisi zenye  nguvu  na ushawishi  wa uwezo wa kuweza kubadilisha  vitu duniani hususani   maendeleo ya  teknolojia  ya habari  na mawasiliano na uwepo wa asilimia kubwa za  wantazania   waliozaliwa  mwaka 2001  huku sera hiyo ikiwa imependekezwa.


Kutokana na  hali hiyo  wizara  imeona  vyema  kufanya maboresho  ya sera hiyo ili kuweza kutoa  nafasi   kwa wantazania wote na kutoa maoni yao juu ya sera hiyo  na kuunda kesho   yao ili kuendana na  wakati   wa sasa na wakati ujao.


Naye Naibu  waziri  wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki    Balozi  Mbarouk    Nassor   Mbarouk  amesema msimamo wa Tanzania ni ule ule toka enzi  za  Hayati  mwalimu  Julius  kambarage  nyerere ni kushikamana na kuendeleza umoja katika kukuza sera nchini.


Kongamano hilo  la kukusanya maoni ya wadau mablimbali ambao wamehudhuria litaenda kuleta chachu katika maendeleo ya nchi na kuibua  viongozi Mahiri wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini  wasomi na viongozi  wa Dini kutoka mikoa  Mbalimbali nchini.







Post a Comment

0 Comments