Na Sheila Ahmadi
Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi imeaandaa Mpango Mkuu (Master Plan) wa Miundombinu ya nchi kulingana na mahitaji ya kiuchumi na kijamii itakayoweza kurahisisha usafiri na usafrishaji wa bidhaa kutoka sehemu mbalimabli kulingana na ongezeko la watu nchini.
Mpango huo unaenda kulenga sababu mahususi kuhusu suala nzima la barabara wa nchi nzima kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA).
hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa, Jijini dar es salaam wakati alipokutana na Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafiri na Utalii kutoka nchi ya Japan, Mhe. Konosuke Kokuba ambaye ameongozana na watalaamu mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi nchini Japani.
“Miundombinu hiyo ya barabara inaenda kuleta mafanikio huku miundombinu mingine ikiendelea kufanya kazi kwa wananchi ikiwemo reli, hivyo tunaenda kushirikiana kwenye Wizara ya Uchukuzi ili kwenda kuandaa master plan ya miundombinu katika kuweza kuhudumia watanzania”, amesema Waziri Bashungwa
Aidha bashungwa ametoa wito kwa TANROADS katika kuandaa majadiliano muhimu na Wakandarasi husika kutoka Tanzania na nchi ya Japani ambapo watakuwa endelevu katika.kuendeleza ushirikiano wa karibu katika Sekta hiyo.
Waziri Bashungwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo ya kuweka mazingira wezeshi kwa Wakandarasi Wazawa ambapo Wizara imeanza kupitia mpango wa manunuzi ambao Mwanzo ulikuwa unawakwamisha wakandarasi hao.
Katika hatua nyingine Waziri Bashungwa amepongeza Serikali ya Japani kwa kwa kuonesha ushirikiano Mahiri baina ya nchi hizo mbili ambazo ni Tanzania na Japan hivyo nchi ya Tanzania itaendelea kuzialika Sekta Binafsi kutoka nchi hiyo ili kuweza kuendelea kufanya kazi na mkampuni ya Tanzania kwa karibu zaidi ili kubadilishana uzoefu wa kazi
Bashungwa amesema Dhamira ya Waziri huyo ni kuja kwa muda sahihi kwani Serikali inaenda kuboresha Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kama mdau mkubwa wa matengenezo ya magari aina ya TOYOTA ambayo kwa asilimia kubwa yanatumika Serikalini na kuhitaji msaada wa kiufundi (Technical Assisatant).
Naye , Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafiri na Utalii kutoka Serikali ya Japan, Mhe. Konosuke Kokuba, amesema Serikali hiyo itaendelea kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili kwa kuendelea kujenga miundombinu yenye ubora katika miradi mbalimbali inayoendelea na ambayo inatarajiwa kutekelezwa hivi karibuni
Amesema kutokana na ongezeko la watu katika nchi zinazokuwa zinahitaji teknolojia za kisasa katika ujenzi wa miundombinu nchini ili ziweze kutosheleza kwa mahitaji muhimu kwa watumiaji
Sanjari na hayo Mkutano huo umeweza kukutanisha Taasisi za Wakala wa Barabara (TANROADS), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Wakala wa Majengo (TBA) na Jumuiya ya Maendeleo ya Miundombinu ya Japani - Afrika (JAIDA).



0 Comments