Na Sheila Ahamadi
Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani limewataka wamiliki na madereva wa gari na pikipiki wote nchi kutoweka vingora, vimulimuli, namba za bandia na taa za kuongezwa kwenye magari na pikipiki kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria, taratibu na kanuni za usalama Barabarani.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani DCP Othman Nga’nzi Wakati akizungumza na waandishi wa Habari na kubainisha kuwa Kuna baadhi ya watu wamejenga utamaduni wa kujihalalishia kuwa ni Sheria kuweka namba za bandia kwenye magari Yao.
Kamanda wa jeshi hilo amewashauri. wamiliki wa vyombo vya moto na madereva ambao wanafunga vingora, vimulimuli namba za bandia na taa za kuongezwa kwenye magari na pikipiki kama Kuna ulazima wa kufanya hivyo basi wanatakiwa kuomba na kupata ridhaa ya kufanya hivyo kutoka Kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ndie mwenye dhamana ya kuidhinisha vibali hivyo.
“kuna baadhi ya watu binafsi makampuni au taasisi zinafunga vingora katika magari yao na kubitumia bila kuzingatia utaratibu wa kisheria, Kwa kufanya hivyo Wanavunja sheria ya usalama Barabarani na wanastahili adhabu ikiwemo ya kulipia faini ya tozo za makosa ya usalama Barabarani au kuweka mahabusu na kuandaliwa mashtaka na kupelekwa mahakamani au vyote Kwa pamoja” Amesema DCP Nga’nzi
Aidha Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani tutaanza oparesheni kabambe ya kukamata magari yote ambayo si ya dharura na yamefungwa vingora bila kuzingatia utaratibu wa kisheria “
Vilevile Nga’nzi amefafanua kuwa wananchi wanapaswa kujua kuwa taa zilizowekwa kutoka kiwandani zinaruhusiwa kisheria mfano magari ya mgodini na kuwindia porini lakini matumizi yake yawe sehemu husika.
Kuna Sheria za Usalama Barabarani sura ya 168 kama ilivyopitiwa mwaka 2002 kifungu Cha 54 (2) (5) kingora kitafungwa kwenye gari au pikipiki za dharura, mfano magari na pikipiki zitumikazo katika misafara ya viongozi, pikipiki za polisi, Zimamoto, hospitali na pikipiki za Jeshi tena kwa kuzingatia maelekezo ya Waziri mwenye dhamana ya Usalama Barabarani.

0 Comments