Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile ameitaka mamlaka wa viwanja vya ndege Tanzania (TAA) kuvunja mkataba na Mkandarasi anayejenga jengo la abiria la kiwanja cha ndege cha Ruvuma kutoka na Mkandarasi huyo kushindwa kukamilisha jengo hilo kwa wakati.
Kihenzile ameyasema hayo Mara baada ya kutembelea na kukagua maboresho makubwa ambayo yameweza kufanywa kwenye uwanja wa Ndege wa Songea mkoani ruvuma.
“Aidha Naibu waziri huyo amesema kuwa Serikali imewekeza bilioni 37 katika uwanja wa ndege huu, hivyo ni muhimu jengo la abiria likamilike kwa haraka. Nauelekeza uongozi wa TAA kuvunja mkataba na Mkandarasi anayejenga Jengo la Abiria kwani ameshindwa kukamilisha kwa wakati ,Alisema Kihenzile
Jengo hilo la abiria lilitakiwa kukamilika mwezi wa sita mwaka jana lakini mpaka sasa lipo asilimia 30 na Ujenzi wake unathamani ya shilingi milioni mianne ishirini na tatu (423) huku ujenzi ukiwa umesimama kutokana na changamoto za mkandarasi huyo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amesema kuwa uwanja wa Ndege wa Songea ni muhimu kwa usafirishaji wa Mizigo na Abiria kutoka nchi jirani kama vile Msumbiji na Malawi hivyo usafirishaji wa mazao ya Mboga mboga na matunda kama vile parachichi hivyo wananchi wa Songea na Mikoa jirani ni Muhimu kutumia uwanja huu ,alisema Ndile
Awali Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songea Mhandisi Danstan Komba akisoma taarifa ya uwanja wa ndege huo amesema kuwa ujenzi wa Barabara ya ndege (Run way) umekamilika ,ujenzi wa barabara ya kiungio (Taxing Way) umekalika,Ujenzi wa kituo cha nishati umeweza kukamilika hivyo bado jengo la abiria .
Hata hivyo uwanja wa ndege wa Songea ni mojawapo ya viwanja vya ndege vilivyojengwa kuanzia mwaka 1974 kikiwa na barabara ya kutokana na kuruka ndege kwa kiwango cha changarawe, lakini sasa serikali umeboresha uwanja huo na kuwa uwanja wa kisasa.






0 Comments