SHIRIKA LA NDEGE LA AIR TANZANIA LATOA UFAFANUZI WA NDEGE ILIYOPATA HITILAFU MWAKA HUU.

 

Na Sheila Ahmadi

Shirika la ndege la Air Tanzania latoa ufafanuzi  wa ndege yenye namba 106  iyopata hitilafu mwaka huu tarehe 24  ambapo ndege hiyo ikitokea mkoani Dar es salam kwenda mkoani mbeya Shirika hilo limesema kuwa hitilafu kwenye chombo cha moto huwa ni kawaida kutokea hivyo baada ya hitilafu kutokea tuliweza kurudisha ndege hiyo na kuweza kuchukua ndege nyingine ya kwenda mbaya.


Hayo yamesemwa  Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa shirika la ndege la Air Tanzania  Mhandisi  Ladslaus Matindi ameeleza kuwa tumeona kwa sasa ni wakati sahihi wa kutoa taarifa kutokana na shirika la ndege yetu kupata hitilafu kadhaa kwani kuna baadhi ya taarifa zinatolewa ambazo hazina ukweli kuhusiana na hitilafu ambayo imetokea kwenye ndege yetu iliyokua  inaelekea mkoani mbeya.


Ndege yetu iliweza kuondoka sa 12. Mara baada ya nusu saa kulikua na Harufu ya moshi hiyo ilitokana na injini ya ndege hiyo kupata joto Kali  hivyo kupelekea kwa joto hilo ilienda kusababisha hitilafu hiyo moshi huo ulienda kupeleka hewa tofauti kwenye ndege hiyo hivyo sehemu ambayo wamekaa abiria kukawa na moshi ambao ulikua unatoka kwenye injini.


"Abiria wetu walianza kupatwa na hofu ya moshi huo  Huku wafanyakazi  na marubani wa ndege hiyo walianza kuchukua hatua  za kiusalama ambavyo zilifanywa kwa weledi sana huku moshi ukiendelea kwa Tarkribani dakika Tano pia injini ya ndege ilizimwa kwa ajili ya usalama zaidi.


Lakini kwa kuthamini zaidi usalama wa abiria   rubani alirudisha ndege Dar es salaam na ilichukua Dakika 25 toka hitilafu ilipotokea mpaka ndege ilivoweza kurudishwa Dar es salaam na iliweza kutua salama hivyo chombo cha moto ni jambo la kawaida kupata hitilafu ndongondogo kama hii ambayo imetokea kwenye ndege yetu. " Amesema mkurugenzi Mhandisi. Matindi.


Aidha Mkurugenzi matindi  sisi tulipoweza kupata taarifa hiyo ya uongo tulitoa Taarifa ya kweli halisi iliyotokea hivyo  abiria waliupongeza uongozi wa shirika hilo kwa kuweza kutatua changamoto iliyotokea  kwenye ndege hiyo kwa kubadilishiwa ndege nyingine.

Kwa upande wake msimamizi wa ndege hiyo Wiliam  Zorote amesema kuwa tuliweza kuwadhibiti abiria kwa kupatwa na hofu kwenye ndege hiyo mara baada ya hitilafu hiyo ya moshi kuweza kutokea kwenye ndege.


Naye  kaimu mkuu wa usalama  Emmanuel Tivai ameongeza kwa kusema kuwa hitilafu kwenye chombo cha moto ni kawaida kutokea kwani kuna wakati baadhi ya vifaa ikiwemo injini kupata joto Kali.


Sambamba na hayo Mhudumu wa ndege hiyo Mwanaidi  Mwanga ametoa pongezi kwa Mamlaka hiyo kwa kuweza kutoa mafunzo mazuri hivyo hitilafu ya ndege hiyo ilivotokea  waliweza kufanya mambo kadhaa ya kudhibiti changamoto ambazo zingeweza kutokea.

Post a Comment

0 Comments