TANZANIA NA MISRI YAUNGANA KUBORESHA MIUNDOMBINU MBALIMBALI. IKIWEMO BANDARI


Na:  Sheila  Ahmadi


Tanzania na MiSri  yaungana  katika kuboresha miundombinu mbalimabilia ikiwemo bandari hivyo kupitia muungano huo unaenda kuleta mabadiliko ya kimkakati katika kuleta miuondombinu iliyo bora nchini Huku baadhi ya wafanyakazi kutoka wizara ya uchukuzi wakitakiwa kwenda kutembelea Misri kwenda kuangalia miundombinu ya reli za kisasa na za kawaida.


Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar. Es salaam  Waziri wa uchukuzi  Professa Makame mbarawa amesema tumepata mgeni ambae ni Waziri   Alwazeer ambae anashughulikia mambo ya miundombinu  kutoka Misri Huku lengo la ugeni huo ni kuweza kuona miundombinu inavyofanya kazi kwa viwango. Na kuweza kubadlishana ujuzi wa kazi ambazo zinafanywa.


Miundombinu hiyo ikijumuisha Bandari, viwanja vya ndege na barabara za treni hivyo kupitia miundombinu hiyo tunaona tunawekeza kwenye bandari ya Dar es salaam kutoka gati namba moja hadi kufikia gati ya saba na tumeweza kuwakaribisha  wawekezaji wengi Na kuwapa fursa katika kukuza uchumi wa bluu nchini.


Aidha. Waziri mbarawa amesema kuwa  tupo kwenye mkakati wa kuandaa gati maalumu ambalo linaenda kuteremshia mafuta bandarini hivyo kupitia serikali ya awamu ya sita tunasubiri fedha za kutosha ili kuweza kujenga gati hilo ambalo litaenda kurahisisha ushushwaji wa mafuta bandarini.


"Kama mnavofahamu wizara hii imepewa fedha na Rais Dkt Samia suluhu katika kuhakikisha kuwa uchukuzi  na miundombinu mingine inakua  kwa asilimia kubwa kutokana na watu wa misri wamekuwa kiuchumi zaidi ndio maana wamekuja kutembelea bandari ya dar es salam kwani ndio kubwa katika afrika Mashariki na kuona namma gani wanaweza kuwekeza  kwenye bandari yetu.


Kwa sas tuna mradi mkubwa wa ujenzi wa bandari namba 13,14, na 15 kupitia mfumo  uitwao PKP kwa ajili ya ushirikishaji wa sekta binafsi mradi huo ni umuhimu kutokana na kufungua  fursa na kupunguza changamoto za meli ambazo zinatokea kwenye bandari yetu ya dar es salam na sio mda mrefu inaenda kuonesha fursa kwa wawekezaji wengine.   " Amesema  Waziri  mbarawa"


Pia Kuna baadhi ya miradi ipatikanayo Mkoani tanga  na. Mtwara lakini hawatoweza kufika kwani waataalamu wengine wameweza kueleza miradi mingine kutoka Mtwara mpaka mbambabay na bado hatujaweza kupata wawekezaji na mradi mwingine wa Kaliua napo bado hatujafanikiwa kupata wawekezaji.


Naye waziri  Kamel Alwazeer  anaeshuhulikia miundombinu kutoka misri amesema kuwa tumekuja Tanzania ili kuweza kuendeleza biashara  na uboreshaji wa miundombinu kwani itaenda kupelekea ukuaji wa miradi katika kujenga bandari kavu kwani ndio nchi pekee ambayo ni kitovu cha uwepo wa bandari nyingi zaidi.


Nimefurahi kuja kutembea Nchini Tanzania hivyo ninawakaribisha wizara ya uchukuzi. Akiwemo waziri  mbarawa  kuja kutembea nchini kwetu ili kwenda kuona baadhi ya miundombinu inayotumiwa katika kuleta Maendeleo  hivyo Nina imani kuwa ujio huu unaenda kufungua biashara kwa wigo mkubwa. " Amesema jenerali  Alwazeer










Post a Comment

0 Comments