WIZARA YA UCHUKUZI IMEWATAKA WANANCHI KUPATA FURSA KUPITIA UJENZI WA MANTEKI YA MAFUTA.

   

Na. Sheila  Ahmadi



Waziri wa Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa amewataka   wananchi   kuweza  kuchangamkia fursa  ambazo zitaweza kuzaa matunda  kupitia kwenye  mradi wa ujenzi  wa matenki 15 na miundombinu ya kupokea, kuhifadhi na kusambaza bidhaa za mafuta huku akitaka wawe waadilifu na kuweke uzalendo mbele.






Waziri   mbarawa  amewataka  Mamlaka ya bandari. TPA na wizara ya Uchukuzi  kuweza kufanya  kazi kwa makini  huku miradi hiyo iweze  kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuendana na thamani halisi ya fedha ya mradi husika.


Ameyasema hayo jijini. Dar es salaam Mara baada ya  hafla ya utiaji saini  wa mkataba wa mradi wa usanifu na ujenzi wa matenki na miundombinu ya kupokea,kuhifadhi na kusambaza bidhaa za mafuta ya petroli katika bandari ya Dar es salaam.



"Amesema kuwa  utiaji saini wa mkataba huu ni suala Mahususi   kwa nchi kwani ni zaidi ya miaka 10 tumekuwa. Tukifanya kazi na kuandaa fedha za ujenzi huo na kukuza mradi wetu ambao unaenda kuleta maendeleo na uchumi wa bluu.




Vilevile  Amehakikisha  kuwa mradi huo  unaenda kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 678.6 ambazo yataenda  kupewa Mkandarasi  ambae anahusika na ujenzi huo M/S China Railway Major Bridge Engineering Group Co. Ltd. na M/S WUHUAN Engineering Co. Ltd, ya china ilipendekezwa kupewa zabuni. " Amesema  Waziri Mbarawa"



Naye  mkurugenzi mkuu mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Plasduce Mbossa amesema ujenzi wa tanki hizo itaenda  kusaidia Kupungua kwa gharama ambazo  zinazotokana na meli kukaa bandarini  kwa muda mrefu (demurrage charges) kwani kwa sasa meli za SPM zinatumia wastani wa siku 11 mpaka 12 kushusha mafuta ambapo kwa sasa kushusha unatumia dola za kimarekani 25,000 kwa siku.





Aidha   Mkurugenzi. Mbosa ameongeza kuwa  Ujenzi wa matenki unategemewa  kwenda kurahisisha ushushaji wa mafuta na kupunguza hadi siku 3 mpaka 4. Hii itaendana  na hali ya sasa kwani  wanatumia masaa 48 kushusha mafuta melini kupitia SPM. Kwa maana nyingine, kutakuwa na saving ya wastani wa siku 8 ambazo ni sawa na dola za kimarekani 200,000 (US$ 25,000 x 8). Kwa kuwa gharama hii kwa sasa inakwenda kwenye bei ya pump, hali hii pia inategemewa kupunguza bei ya mafuta kwa mwananchi wa kawaida.



“Ujenzi wa haya matanki 15 unaenda kusaidia baadhi. Ya uimara  wa ukusanyaji wa mapato. Kwa kuwa mafuta yote yatapokelewa na kupimwa vizuri yakiwa sehemu moja (tank farms) na kuwa chini ya Mamlaka ya Bandari kabla ya kuyasambaza, hali hii itaimarisha udhibiti wa mapato ya Serikali kwa kuzuia mianya ya ukwepaji kodi na kurahisisha ukusanyaji wa mapato yatokanayo na bidhaa za mafuta zinazoingia nchini”,Amesema.  Mkurugenzi mbosa



Sanjari na hayo amesema kuwa Ujenzi wa matenki hayo ya mafuta pia yatahakikisha usalama wa uwepo wa mafuta (security of supply) na pia itasaidia uanzishwaji wa Strategic Petroleum Reserve (SPR). Kwa kuwa mafuta ni moja ya bidhaa ambayo inachangia kiasi kikubwa cha exchange rate, uwepo wa SPR utaleta uimara wa sarafu ya Tanzania dhidi ya dola za kimarekani.





“Uwepo wa uhakika wa mafuta nchini kutokana na ujenzi wa tank farms and gati la kupokea na kupakua mafuta pia inaweza kupunguza mfumuko wa bei (inflation) na kuleta nafuu kwa mwananchi wa kawaida. Hii inatokana na ukweli kwamba kupanda kwa bei ya mafuta kunasababisha kwa kiasi kikubwa kupanda kwa bidhaa nyingine,”Amesema Mbossa.


Pia  ameongeza kuwa Mradi utachochea mashirika yanayoshughulika na mafuta kuanzisha Kituo cha usambazaji Mafuta (Hub) kwenda nchi za jirani kama vile Uganda, Rwanda, Burundi, Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo na hivyo kuifanya Tanzania kua kituo cha soko la biashara


Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu ametoa wito  kwa wizara ya uchukuzi na mamalaka ya bandari  TPA kuhakikisha mradi huo pindi utakapoanza uhakikishe unatoa kipaumbele kwa wananchi wazawa ili waweze kupata ajira



Post a Comment

0 Comments