Na Sheila Ahmadi
Mtendaji kuu wa Wakala wa Barabara Tanzania Mhandisi Mohamed Besta ametoa wito kwenye Sekta ya ujenzi kuweza kutekeleza majukumu ya kazi kwa kushirikiana.
Hayo yamesemwa jijini dar es salam na mhandisi besta mara baada ya kyzungumza na WAHANDISI na wa vyuo mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku ya Uhandisi Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
maadhimisho haya yameandaliwa na Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) kwa kushirikiana na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) na Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania (ACET) amesema ushirikiano huo ni kwasababu mara nyingi suluhisho za matatizo mengi katika jamii zinagunduliwa na wahandisi na mafundi ambao wanafanya kazi hiyo.
"Vyuo vikuu ambao mpo hapa, nyie mnauwezo wa kufanya tafiti na kushauri njia bora na endelevu za kutatua changamoto hizo. Lakini wanafunzi pia mpo hapa. Naamini jamii ikiwashirikisha na kuwatumia ipasavyo mnaweza kuja na suluhisho za changamoto nyingi sana katika jamii yetu, tunachopaswa kufanya ni kubadili fikra yaani mindset," amesema Mhandisi Besta.
Aidha amesema kuwa kuhusu maadhimisho hayo, Mhandisi Besta ameeleza kuwa Wahandisi kupitia taasisi za Wahandisi Dunia nzima wanakutana katika siku ya leo ili kubadilishana uzoefu na kuonesha nini kinafanywa na wadau wa uhandisi ili kuwa na ulimwengu endelevu.
Dhumuni la taasisi hizo tatu IET, ACET NA ERB kuadhimia kualika makundi tofauti tofauti katika maadhimisho hayo kama vile wadhibiti, wakala, watoa huduma na wanafunzi ni kujadili dhana ya kujenga utamaduni wa kufikiri tofauti ili kupata suluhu kwa matatizo au changamoto zilizopo katika jamii badala ya kusubiri watu wa mataifa mengine kufikiri kwa niaba yetu.
"Wito wangu ni kwamba tukijenga utamaduni huu, Taifa litazaa wahandisi, mafundi na wanasayansi wengi ambao wanatoa suluhu za changamoto zao na zajamii husika," ameongeza Mhandisi Besta.
Kuhusu wanafunzi, Mhandisi Besta ameshauri IET na vyuo watilie mkazo maadhimisho ya kibunifu ambayo yatawavutia wanafunzi kutoka katika shule hizo kushiriki na kupata muamko wa kuwa na bunifu.
Vilevile amewashauri IET waangalie namna ya kuwapata wadau ambao wataweza kuendeleza bunifu hizo ili zifika mwisho na zianze kuleta faida.
Aidha kwamba ili ubunifu wa kiuhandisi uweze kunufaisha nchi yetu, Wahandisi na wataalam wengine nchini wanapaswa kufanya kazi kwa kushirikiana na kukubali kutumia teknolojia za kisasa.
Hata hivyo amesema ili Taifa liweze kujitegemea inabidi wahandisi wawe watafiti na wabunifu ili kuanzisha mifumo yetu wenyewe ya kiteknolojia ambayo itakuwa endelevu. Pia kunapaswa kutengenezwa kiungo kati ya taasisi za elimu na mashirika ili bunifu ziweze kutumiwa na kuleta tija ya kutatua changamoto zilizopo kwa urahisi bila kutegemea nchi zilizoendelea.
Naye Rais wa IET Mhandisi Dkt. Gemma Modu, amesema lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuufahamisha umma ni nini wahandisi na wadau wa uhandisi wanafanya, lakini pia kuwahamasisha vijana wakike na wakiume kupenda na kusoma masomo ya sayansi na hisabati ambayo yanawapelekea kusoma masomo ya uhandisi na ufundi.

0 Comments