Na Sheila. Ahmadi
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linaendelea na operesheni kali maalum ya kuzuia vitendo vya kihalifu na kukamata watuhumiwa mbalimbali wakiwemo wezi wa pikikipi na kukamata pikipiki zilizoibwa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
Operesheni hiyo ilianza tarehe 06 Februari 2024 na inaendelea mpaka sasa imemkamata Omari Mlopa (28) mkazi wa Mlandizi na wenzake wawili wakiwa na pikipiki 32 zilizoibwa na baadae kuzifanya zao kwa kuzikodisha kwa mikataba kwa watu mbalimbali na kujipatia pesa kila siku.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi Kanda maaluma ya Dar es Salaam umebaini kuwa watuhuhumiwa hao walibadilisha namba za usajili za pikipiki hizo na kuweka namba bandia ili zisitambulike.
Kama Nada Muliro ameongeza kuwa Pikipiki 13 tayari zimetambuliwa na wamiliki wake hivyo utaratibu utafuatwa ili wapewe pikipiki zao.
"Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linaendelea operesheni maalum ya ukamataji wa watu wanaokiuka sheria kwa kutenda makosa ya usalama barabarani hasa kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) na Bajaji.
Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2023 makosa ya pikipiki yaliyokamatwa ni 179,174, walioandikiwa faini za papo kwa hapo ni 178,937, waliofikishwa Mahakamani ni 237, waliohukumiwa adhabu ya kulipa faini 236, na mmoja alihukumiwa kifungo jela.
Kwa kipindi cha Januari hadi Februari 2024 makosa ya pikipiki yaliyokamatwa 36,775, walioandikiwa faini za papo kwa hapo ni 36,754, waliofikishwa mahakamani ni 14, na mashauri 7 yapo kwenye ofisi ya Mashitaka ya Taifa.
Katika Operesheni hii baadhi ya makosa ambayo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara kwa waendesha pikipiki na bajaji ni kutovaa kofia ngumu, kupita taa nyekundu, ulevi, kuzidisha abiria, kupita barabara za mabasi yaendayo haraka pamoja na kupakia abiria kwenye taa za kuongozea magari.
Aidha amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam licha ya kuendelea kutoa elimu juu ya uzuiaji wa makosa, ukamataji umelenga pia watu ambao wamekuwa wakikaidi na kutotii sheria kwa kuendesha vyombo vya moto bila kujali na baadae kujikuta wakisababisha ajali.
Watuhumiwa 59 mbaroni kwa makosa ya kihalifu akiwemo muuzaji sugu wa dawa za kulevya aina ya bangi.
0 Comments