WIZARA YA UCHUKUZI INATARAJIA KUJENGA GATI JIPYA MKOANI MTWARA ITAKAYOHUDUMIA MAKAA YA MAWE, SIMENT BANDARINI.

 

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali inaendelea kununua mitambo ya kisasa kwa ajili ya kuhudumia Bandari ya Mtwara pia kujenga Gati jipya  eneo la kisiwa Mgao kwa ajili ya kuhudumia bidhaa za Makaa ya Mawe, Cement na Mbolea.


Mbarawa amaeyasema hayo Baada ya kukagua  utendaji kazi wa Bandari ya Mtwara Pamoja kutembelea eneo la Kisiwa Mgao ambapo panatarajiwa kujengwa geti jipya.


“Serikali ipo katika hatua ya Mwisho ya kutafuta  na kupata mkandarasi wa kujenga gati jipya katika eneo la kisiwa Mgao ili gati hilo liweze kuhudumia bidhaa kama vile Makaa ya Mawe, Sement na Mbolea” Alisema  Prof. Mbarawa.


Aidha  Prof  Mbarawa amesema kuwa uboreshaji wa Bandari ya Mtwara umeongeza fursa kwa vijana kupata ajira pia mzunguko wa fedha umeongeza .



Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Newala  Rajab Kundya amesema kuwa kutokana  na kuongezeka kwa uafanisi katika Bandari ya Mtwara kuna  fursa kwa vijana wa Mtwara ambapo imeweza  kuongezeka  kwa kiasi kikubwa   na kufanya Mtwara vijana wengi kujishughulisha  na kazi mbalimbali.


 “sambamba na hayo ameongeza kwa kusema kuwa uboreshaji wa Bandari ya Mtwara umevutia nchi ya Msumbiji na Visiwa vya Comoro  kwa kutumia bandari hiyo kwa ajili ya kusafirsha bidhaa mbalimbali kama vile Sement  mazao ya chakula”Alisema Rajab Kundya



Naye  Meneja wa Bandari ya Mtwara Ferdinand Nyathi amsema kuwa  pamoja na Bandari hiyo kusafarisha Korosho lakini serikali imenunua mitambo ya shilingi Bilioni 36 kwa ajili ya kuhudumia bidhaa Mchanganyiko na tayari mtambo huo  umeshawasili katika Bandari ya Mtwara na Mtambo mwingine unatarajia kuwasili mwishoni mwa mwezi huu.

Post a Comment

0 Comments