NA VICTOR MASANGU,PWANI
WAKALA wa huduma za Misitu Tanzania ( TFS ) wametoa hundi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokumbwa na mafuriko katika Wilaya za Rufiji na Kibiti mkoa wa Pwani na makazi yao kuzingirwa na maji.
Akipokea msaada huo mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewashukuru TFS na kubainisha kwamba bado kuna uhitaji mkubwa hivyo fedha hizo zitakwenda kuwa msaada mkubwa katika kutatua changamoto zilizowakabili wananchi hao.
Kunenge aliwapongeza kwa dhati kwa kutoa msaada huo wa fedha ambazo zitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwafikishia huduma na mahitaji mbali mbali.
"Nawashukuru sana TFS kwa kuweza kutoa fedha hii na zitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupelela huduma kwa wananchi ambao wamekumbwa na mafuriko katika Wilaya ya Rufiji na Kibiti,"alisema Kunenge.
Kadhalika kunenge aliwahimiza wananchi kuondoka katika maeneo ambayo ni hatarishi na kuweza kuhamia katika maeneo ambayo ni salama ambayo yametengwa na serikali.
Akikabidhi msaada huo Meneja uhusiano wa TFS amesema kwamba Johari Kachambwa amesema wameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa na athari za mafuriko yaliyotokea.
Johari alisema kuwa ana imani kwamba fedha hizo walizozitoa ana imani kubwa zitaweza kuwasaidia wananchi hao katika mahitaji yao mbali mbali.
"Sisi kama TFS tumeguswa sana na wenzetu ambao ni wananchi wa Wilaya ya Rufiji na Kibiti na tumemkabidhi mkuu wa Mkoa wa Pwani mfano wa hundi ya kiasi cha shilingi 20,"alisemwa Kachambwa.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema maandalizi kwa ajili ya kuupokea Mwenge yamekamilika na kuwahimiza wananchi kujitoza kwa wingi April 29 mwaka huu katika halmashauri ya Chalinze.

0 Comments