MCHAMBUZI WA SIASA KASSIM KIBAO AFAFANUA SUALA LA UPOTOSHAJI UMMA KUTOKA KWA MBUNGE MPINA.

 

Na  Mwandishi   Wetu.

 Mchambuzi wa maswala ya  Siasa na uchumi Nchini, Bwana Kasim kibao Amesema kuwa  mbunge wa kisesa Ndug  luhaga mpina amefanya  kitendo cha  kupotosha umma  juu ya tuhuma alizozitoa kwa Waziri Wa  kilimo na chakula Mheshimiwa Hussein bashe ambapo amemtuhumu kwa kumuita fisadi kufuatia kutoa vibari vya uagizaji sukari kwa wafanyabiashara Biashara.


Hayo yamesemwa  Jijini dar es salaam, na mchambuzi. Wa masuala ya kisiasa  Kassim Kibao ambapo  amesema  kuwa kitendo alichofanya mh.mpina ni kukosa subra kwani alipaswa kufuata ushahuri wa Mheshimiwa spika bunge la jamhuri ya Muungano WA Tanzania Tulia Akson ambaye alimtaka kuleta ushahidi juu ya tuhuma hizo na nyingine mbalimbali.


Sanjari  na hayo Kibao amesema kuwa  kitendo kinachofanywa na mbunge huyo  ni  upotoshaji wa umma na  kuleta taharuki kwa Wananchi jambo ambalo amesema ni kinyume na taratibu na Sheria za nchi.


Aidha. Kibao Amesema anachokifanya Mhe. mpina ni kutafuta huruma kwa Wananchi jambo ambalo  sio  nzuri   kwani   halina afya kwa Taifa  letu la Tanzania.


Vilevile  Kibao ameongeza kuwa kuhusu sakata Mheshimiwa Waziri  wa  kilimo mhe  bashe ambaye aliagiza  Wizara ya kilimo kutoa vibali  kwa wafanyabiashara wa viwanda ili Kuokoa hali ya sukari Nchini katika kipindi cha mwezi mtukufu Wa  Ramadhan na kwarezima.

Post a Comment

0 Comments