Na Mwandishi wetu
Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatarajiwa kufanya maadhimisho makubwa ya kusheherekea miaka 60 tangu kuasisiwa Kwa Jeshi hilo na Baba wa Taifa,Hayati Julius Kambarage Nyerere.
Hayo yamesemwa Jijini Dar Es Salaam, na Kaimu mkurugenzi wa Habari Uhusiano ,na msemaji wa JWTZ,Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika septemba 1,2024 ambapo pia yataenda sambamba na zoezi kubwa la kivita ambalo halijawahi kufanyika tangu kuanzishwa kwake.
Luteni Kanali Ilonda amesema kuwa zoezi hilo Kubwa litashirikisha kamandi zote za Jeshi hilo ikiwemo,kamandi ya Jeshi la kujenga Taifa,Jeshi la anga,Jeshi ardhini,na Jeshi la majini katika Mikoa ya Morogoro,Tanga,Pwani na Dar Es Salaam ambapo zoezi hilo litahusisha mapigo ya ardhini,angani na baharini ambayo yataanza kuanzia Julai 25 Hadi Agosti 25 mwaka huu katika Mikoa hiyo.
Aidha maadhimisho hayo pia yataambatana na zoezi la upimaji,ushauri na matibabu ya huduma za Afya Kwa wananchi bila Malipo katika hospitali za Jeshi za kanda za Arusha,Mwanza,Mbeya,Tabora na Zanzibar ambapo wananchi watakapofika katika hospitali hizo watapata vipimo na matibabu bure.
"Sisi. Kama JWTZ tunasheherekea miaka 60 tangu Jeshi lilipoasisiwa mnamo Septemba 1 mwaka 1964 na mpaka Sasa ikiwa nchi Ina utulivu na amani tumeona pia tusheherekee na wananchi wetu kwa Jeshi kuwapa huduma za Afya ikiwemo vipimo na matibabu bure kwani pia tumetenga eneo la upimaji na matibabu bure pale uwanja wa Zachiem,Mbagala,Mapinga Bagamoyo na Visiwani Pemba pia"amesema Kanali Ilonda.
Vilevile. amesema kuwa. katika maadhimisho hayo ya miaka 60 ya JWTZ yataambatana na mashindano makubwa ya utamaduni ya Mkuu wa majeshi ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo ambayo yana lengo ka kukuza utamaduni wa watanzania ambapo pia yataambatana na mashindano ya Michezo mbalimbali ya Mkuu wa majeshi yajulikanayo kama CDF CUP.
"kupitia. maadhimisho haya pia Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ litafanya gwaride kubwa litakaloongozwa na onyesho la dhana mbalimbali za kivita tangu kuanza Kwa Jeshi mwaka 1964 mpaka Sasa".ameongeza
Sanjari. Na hayo miaka 60 ya JWTZ yanafanyika na kauli mbiu isemayo,'miaka 60 ya JWTZ umoja,nidhamu,utii na uhodari ni Msingi wa jeshi letu katika kudumisha ulinzi,amani na utulivu'
Katika Hatua nyingine ameongeza kuwa Jeshi la wananchi wa Tanzania liliasisiwa rasmi na kuanza mnamo mwaka 1964 na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere .

0 Comments