Na Mwandishi wetu
Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amesema ameridhishwa na uendeshwaji wa treni ya kisasa kwa kipande cha Dar-Moro na maendeleo ya ukamilishwaji wa miundombinu ya kipande cha Moro-Dom
Prof Mbarawa ameyasema hayo wakati wa Ziara ya kukagua maendeleo ya safari za treni ya kisasa kutoka Dar-Moro kwa kutumia treni hiyo na baadae kukagua ukamilishwaji wa miundombinu kwa kipande cha Moro-Dom Leo tarehe 03 July, 2024
"Ziara yangu imeanzia Dar es salaam Leo saa kumi na mbili asubuh mpaka morogoro kwa ajili ya kuangalia uendeshwaji wa treni ya kisasa, changamoto, pamoja na kujifunza kwa kutumia Treni ya kisasa na sehemu ya pili ni kuangalia matayarisho ya miundombinu kutoka Moro-Dom kwa kutumia kiberenge ili kukagua utayari wa kuanza safari za moja kwa moja mwezi huu" amesema Mbarawa
Ameongeza kuwa kwa kipande cha Moro-Dom mambo machache ambayo hayajakamilika ni ufungaji wa senyenge ambao utakamilika baada ya siku 8, miundombinu wezeshi yote kukamilika ndani ya wiki moja vile vile madereva wengi wanafanya majaribio kwa ajili ya njia hiyo, nauli zimeshapangwa kwa njia zote na Wananchi wameridhika nazo
Amesema Stesheni zote Kuanzia Kilosa mpaka Dodoma zimekamilika kwa asilimia Mia moja,mifumo ya tiketi bado kufungwa tu hivyo kama waziri mwenye dhamana ameridhika na kazi iliyofanyika na anaamini pasipo shaka tarehe 25 July,2024 treni itaanza kupita
Awali akiwa ameambatana na Waziri wa Uchukuzi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima ameishukuru Trc na Wizara kwa kuendelea kuongeza idadi ya treni zinazofanya safari kipande cha Dar-Moro kwani abiria wamefurahia sana uwepo wa treni hii na kwa hakika itakuza sana uchumi wa mkoa na kuongeza pato la Taifa
Akitoa salam za Shirika Kaimu Mkurugenzi wa TRC Mha Machibya Shiwa amesema safari ya ujenzi wa reli ya kisasa nchini ilianza mwaka 2017 na leo hii reli inapoanza kutumika ni faraja kubwa kwa shirika na wanapata hamasa ya kuendelea na ujenzi kwa maeneo mengine
Ameongeza kuwa kwa wananchi wa Dodoma Shirika liko tayari kuanza kuwapa huduma kuanzia tarehe 25 July,2024 maana maeneo makubwa ya kihandisi shirika limejiridhisha reli hii kwa kipande cha Morogoro-Dodoma na kuelekea Dar es salaam inaweza ikatumika na tayari majaribio mengi yamefanyika kwa upande wa vitendea kazi pamoja na njia





0 Comments