MBUNGE KOKA APIGA JEKI ML.5 SHULE YA MSINGI SAINI



VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka  katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu ametumia fedha za mfuko wa Jimbo kiasi cha shilingi milioni tano katika mradi wa ujenzi wa shule ya msingi shikizi ya Saini ili kuondokana na changamoto ya wanafunzi wadogo kutembea umbari mrefu wa zaidi ya kilometa 12.


Hayo yamebainishwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mathias Alexanda wakati akitoa taarifa kwenye ziara ya kikazi ya  Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini ambaye alifika kwa  ajili ya kuweza  kutembelea   miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu pamoja na miundombinu ya barabara.


Mkuu huyo amebainisha kwamba shule hiyo ambayo imeanzishwa  mwaka huu imeweza kuwa ni kombozi mkubwa kwa watoto wadogo wenye umri wa kuanzia miaka mitano na kuendelea kutokana na  hapo awali  wanafunzi hao walikuwa na adha kubwa ya kutembea umbari mrefu kabla ya mradi huo wa shule kuanzishwa.



Mkuu huyo  amempongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni tano ambayo imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha miundombinu ya matundu ya vyoo pamoja na miundombinu mingine ya madarasa katika shule hiyo.


Kwa uapnde wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amebainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuweka mikakati madhubuti ambayo itaweza kusaidia katika kuboresha sekta ya elimu hivyo ameamua kuchangia fedha hizo ili kuwaondolea wanafunzi hao kutembea umbari mrefu.



"Kikubwa nimefarijika kufanya ziaara ya kikazi katika kata ya Visiga na nimetembelea katika shule hii ya awali na darasa la kwanza na la pili la  Saini na nimeweza kujionea mradi huu umeanza utekelezaji wake na ujenzi wa  baahi ya madarasa na mm nimeweza kuchangia kiasi  cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kuboresha   sekta ya elimu ikiwemo madarasa pamojana matundu ya vyoo.

Aidha Mbunge Koka amebainisha kwamba kipaumbele chake kikubwa katika mfuko wa Jimbo ni kuhakikisha kwamba anaboresha zaidi shule ambazo zipo pembezoni ikiwemo kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuweza kuboresha zaidi miundombinu ya madarasa pamoja na maboma ambayo miundombinu yake imechaakaa.

Post a Comment

0 Comments