SERIKALI KUPITIA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) IMESHIRIKIANA NA HESLB KWENYE UREJESHAJI WA MIKOPO.

 

Na  Sheila  Ahmadi

Bodi  ya mikopo ya elimu ya juu  (HESLB) kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wanaenda kushirikiana kwenye uboreshaji, utoaji, na urejeshaji wa mikopo kwa wanufaika nchini.


Akizungumza jijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji Wa bodi ya mikopo ya elimu ya Juu (HESLB) Bill  Kiwia ameipongeza TRA kwakuridhia kushirikiana kwenye urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu hususani utaenda kurahisisha kwa warejeshaji mikopo kupitia kwenye Mamlaka hiyo ya Mapato Tanzania (TRA).


"Sisi kama bodi kazi yetu ni kutoa mikopo  na kuweza kukamilisha zoezi hilo kwa wakati na kupitia ushirikiano huu wa TRA  tunaenda kuboresha huduma zetu  za mikopo kwa wateja wetu ambapo wataweza kuomba mikopo kupitia Mamlaka hiyo." Amesema  Mkurugenzi Kiwia.


Lengo letu la kushirikiana na TRA ni kwenda kutoa huduma kwa wantazania wote  na ziwafikie kwa wakati na kero ya wanafunzi  kuchukua muda mrefu  wa uombaji wa mikopo unaenda kutekelezwa.


Aidha  MKurugenzi  Kiwia ameongeza kuwa tunaenda kubadilishana taarifa Kati ya sisi bodi ya mikopo na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika kurejesha mikopo yetu kwa wanufaika kupitia mikopo hiyo.


Kwa upande  wake Kamishina kutoka Mamlaka ya mapato  nchini Tanzania (TRA) Yusuph  Mwenda amesema kuwa nawapongeza bodi ya mikopo kwa kuweza kutoa mikopo kwa wanafunzi kwani Mikopo hiyo inatokana na walipa kodi kulipa kwa wakati .


Sisi kama Mamlaka ya  mapato nchini Tanzania (TRA) tumeunga mkono. Kwa kuweza kushirikiana kwenye suala madhubuti la urejeshaji wa mikopo na tunaenda kuyatekeleza yote ambayo tumekubaliana kwenye kushirikiana kupitia urejeshaji wa mikopo." Amesema kamishina Mwenda"

Post a Comment

0 Comments