SERIKALI KUPITIA WIZARA YA UCHUKUZI KUFANYA MAPINDUZI YA KIUCHUMI NCHINI.

 

Na Mwandishi  wetu

 Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara amesema sekta ya uchukuzi inaenda kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kutokana na taasisi zake nyingi kufanya vizuri kwenye utekelezaji wa majukumu yao na kuvuka malengo waliojiwekea kuyatimiza kila mwaka ndani ya kipindi cha miaka mitano.



 Prof Kahyarara ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji  wa mkataba wa utekelezaji wa majukumu wa mwaka 2023/24 pamoja na utiaji saini mkataba wa utendaji kazi baina ya taasisi na katibu mkuu kwa mwaka wa 2024/25.



Amesema kuwa taasisi zilizochini ya wizara zimeendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yake jambo ambalo limechangia kuvuka malengo waliyojiwekea kutimiza kila mwaka ndani ya kipindi cha miaka mitano.



“Nadhani sekta yetu kupitia nyie ambao ni watendaji haswa tunakwenda vizuri sana, sisi wengine tunasoma taarifa ya uchumi ya nchi nzima naona kabisa ni jinsi gani sekta inavyochangia uchumi na kwenda kwa kasi kubwa zaidi ya kama tulivyotarajia” alisema Prof Kahyarara.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ufutiliaji na Tathmini  kutoka wizara ya Uchukuzi Devota Gabriel amesema kuwa zoeli la kusaini mikataba kati ya Katibu Mkuu na wakurugenzi wa Taasisi unasidia kukumbushana majukumu muhimu ya utekelezaji wa  kazi kwa kila Taasisi.


 Huku mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Dkt. Tumaini Gurumo kwa upande wake ameeleze siri ya mafanikio ya taasisi hiyo kufanya vizuri ikiwa ni usimamizi mzuri unaofanywa na Wizara ya Uchukuzi, juhudi za taasisi husika kwa kushirikiana na manajement kutimiza malengo  pamoja na ushirikishwaji wa wafanyakazi wa ngazi ya chini ya taasisi.


“usimamizi mzuri unaotolewa na wizara yetu  kwa kuwa tunaposaini huu mkataba tayari tunakua tumeweka ‘commitment’ kwamba tunakwenda kutekeleza sawasawa kwa yale ambayo tumekubaliana, pili ni kwa sisi watekelezaji yaani manajement kutambua majumu yetu kwa pamoja, mwisho ni kwa wafanyakazi wa ngazi ya chini ya taasisi” alisema Dkt Tumaini


Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini(LATRA) CPA. Habibu Suluo amesema  siri kubwa ni mgawanyo wa majukumu , kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja na kufanya ufuatiliaji kujua maendeleo ya utendaji kazi kwa kila idara ndio siri kubwa ya kufikia malengo. 


“ Utaratibu wangu mimi kila wiki nafuatilia kuona kila mkurugenzi ametekeleza kwa kiasi gani lakini pia sisi kila mwezi tunafanya tathmini na kila kikao tunachokifanya ndani ya siku saba za mwanzo wa kila mwezi tunaangalia tumefikia malengo kiasi gani ya katibu mkuu” alisema CPA Suluo


Hata hivyo Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Salim Msangi amesema kama taasisi wataendelea kusiamamia utekelezaji wa sheria za anga za kimataifa pamoja na serikali kama zinavyoelekeza ili ziwawezeshe kufanya vizuri zaidi.


“Tunaongozwa na sheria za kimataifa, sheria zinazofanya anga letu kuwa salama ukiangalia ‘rekodi’ ya Tanzania ni kati ya nchi duniani ambazo  anga lake ni salama  kabisa hivyo tukiendelea kusimamia tutafanya vizuri zaidi” alisema Bw.Msangi

Post a Comment

0 Comments