Na Mwandishi wetu
Waziri wa Uchukuzi Prof .makame Mbarawa amefanya Mazungumzo na Makamu wa waziri wa uchukuzi Mheshimiwa Li Yang, (Vice Minister, Ministry of Transport) kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Prof mbarawa amesema kuwa kutokana na masuala mengine,ya uzalishaji tumejikita zaidi kwenye majadiliano juu ya kuimarisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa njia ya Anga kupitia Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL).
Aidha kama Tunavyofahamu kuwa ndege ya Abiria ya Shirika la ATCL inafanya safari zake kwenda jijini Guangzhou, China mara tatu kwa wiki. hivyo, kutokana na uhitaji kuwa mkubwa, Tanzania imeiomba China kuongeza muda wa ndege hiyo kuweza kuruka kwa siku zote za wiki ili kukidhi haja ya wasafiri wanaotaka kutumia ndege za Kampuni ya ATCL.
Vilevile tumeweza kuwasilisha ombi hilo, na kuweka msisitizo zaidi kwa kuiomba Serikali ya Watu wa China kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China (Civil Aviation Authority of China - CAAC) ili kwenda kurahisisha mchakato wa kutolewa kibali kwa Serikali ya Tanzania cha kurusha ndege ya Mizigo aina ya Boeing 767-300 Freighter yenye uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo kwenda Guangzhou angalau mara tatu kwa wiki. "Alisema Prof Mbarawa"
"Kupitia mazungumzo hayo, Waziri Li Yang ameahidi kuharakishwa kwa mchakato wa upatikanaji wa ridhaa hiyo.
Katika Hatua nyingine mbarawa amesema kuwa kwa Hatua ya upatikanaji wa kibali hicho itakapokamilika huku zoezi la kupeleka ndege ya mizigo nchini China angalau mara tatu kwa wiki itapunguza changamoto ya usafirishaji mizigo ambayo inawakabili Wafanyabiashara wa Kitanzania na kutoka nchi za jirani.
Pia Kikao hicho kimehudhuriwa na Mheshimiwa Khamis Mussa Omar, Balozi wa Tanzania nchini China, Mhandisi Ladislaus Matindi Mkurugenzi Mkuu wa ATCL na Viongozi wengine kutoka Wizara ya Uchukuzi na Taasisi za Wizara.






0 Comments