SERIKALI YA TANZANIA KUSHIRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA USAFIRISHAJI NCHINI CHINA.

 

Na  Mwandishi  wetu

 Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa  ameshiriki  Kongamano la Kimataifa la Usafirishaji Endelevu (2024 Global Sustainable Transport Forum).ambapo  Kongamano hilo  limekutanisha  Mawaziri na Wadau wa masuala usafiri kutoka Mataifa mbalimbali Duniani, huku  likiratibiwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Wizara ya Uchukuzi ya nchi hiyo. 


Akizungumza Kwenye  hadhara hiyo  ya Mkutano  Prof. Mbarawa ameeleza  kuwa mafanikio na hatua mbalimbali ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechukua katika sekta ya usafiri na usafirishaji ikiwemo utekelezaji wa miradi ya reli ya SGR, bandari ,na usafiri wa anga. 


Aidha,  Prof .Mbarawa, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuonesha nia ya kuhusisha reli ya TAZARA ambapo makubaliano yake yalifikiwa tarehe 4 Septemba, Mwaka huu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali katika Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika- FOCAC. Ambapo  Makubaliano hayo yalishuhudiwa na Marais wa Nchi za China, Zambia na Tanzania.



Katika Kongamano hilo Waziri Mbarawa amesema  kuwa  fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya uchukuzi zinazopatikana nchini inatumia  jukwaa hilo kuwakaribisha wawekezaji wenye nia huku akiwahakikishia kuwa, Serikali ya Tanzania imeweka utaratibu mzuri wa kisera wa kushirikiana na Sekta binafsi katika kutekeleza baadhi  ya miradi ikiwemo mradi Bandari na reli ya SGR ili kuwezesha kuifungua nchi zaidi kimaendeleo kupitia utaratibu wa Private Public Partnership (PPP).


Pia  Hatua ambayo inaakisi mpango wa   Maendeleo wa Taifa wa Endelevu wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2030.


Sanjari  na hayo Mbarawa  ameongeza kuwa Kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili tarehe 25 na 26 Septemba, 2024 jijini Beijing, China,  huku Waziri wa Uchukuzi akiwa  ameambatana na Viongozi na Wataalam mbalimbali kutoka Wizarani na Taasisi za Sekta ya Uchukuzi.

Post a Comment

0 Comments