KONGAMANO NNE LA UONGOZI LAFUNGULIWA

 kongamano hilo limekutanisha wanawake viongozi kutoka nchi mbalimbali za barani Afrika wakiwa na lengo  ni kujadili pamoja kuhusu wanawake na uongozi.


Singo amesema kuwa kongamano hilo linafanyika kila mwaka, huku akieleza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya uongozi umeonesha wanawake wengi wapo katika nafasi za chini za utendaji.

“Tumeanzisha program hii ili wanawake wawe na sifa za juu ambazo zitawafanya kuingia katika nafasi za maamuzi, tumeanza kutoa mafunzo tangu mwaka 2022 na kufanikiwa kuhitimu wanawake 199 mpaka sasa” amesema Singo.

Amesema kuwa sasa wanaingia darasa la tano na sita, huku kukiwa na mwitikio mkubwa wa kushiriki kwani zaidi ya wanawake 1,500 waliomba kushiriki lakini nafasi zilizopo 100.

Singo amefafanua kuwa mafunzo hayo yanatolewa bure kwa washiriki, hivyo wanaendelea kutafuta wafadhili ili kuongeza idadi ya washiriki kila mwaka




Post a Comment

0 Comments