WIZARA YA AFYA YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UGONJWA WA MPOX NA MARBURG

 


Na mwandishi wetu

Wizara.  ya  Afya imewatoa mafunzo kwa waandishi wa habari na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusu ugonjwa wa Mpox na Marburg ili kuweza kutoa elimu kwa jamii namna yakujikinga na kuchukua tahadhari.


Mafunzo hayo yamefanyika Oktoba 4,2024 katika Ukumbi wa CTC Hospitali ya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.


Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa sehemu ya Afya kwa Umma Dkt.Ona Machangu amewataka wanahabari na wahariri kutumia kalamu zao kuweza kufikishia jamii elimu juu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko.


"Wanahabari na wahariri wote tuelimishe na kuhamasisha jamii kuweza kufuata hatua mbalimbali za kujikinga kama kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kuepuka kushikana mikono",amesema Dkt.Ona


Hata hivyo Dkt.Ona ameishauri jamii kuendelea kujikinga na kuchukua tahadhari ili kujikinga na magonjwa hayo kwani tayari nchi jirani zina maambukizi ya magonjwa hayo.


Aidha Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha mawasiliano serikalini katika Wizara ya Afya Englibert Kayombo amesema semina hiyo ya waandishi wa habari ni endelevu na taratibu za wizara kukaa pamoja na wadau hao ili kuwapa elimu muhimu itakayosaidia kutoa taarifa kwa usahihi.


Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo James Mhilu amewata waandishi wa habari na wahariri kuwakumbusha wananchi kupiga namba 199 kituo cha miito ya simu cha Wizara ya Afya kwa taarifa,maoni na ushauri.

Post a Comment

0 Comments