AIRTEL YAZINDUA DUKA LAKE NDANI YA STESHENI YA SGR , DAR ES SALAAM

Airtel Tanzania Yapongeza Serikali kwa Uwekezaji wa Miundombinu, Yafungua Duka Jipya katika Kituo cha SGR Dar es Salaam




Airtel Tanzania imeipongeza serikali ya awamu ya sita kwa uwekezaji wenye maono katika miundombinu, hali inayosaidia kuleta mapinduzi katika sekta ya mawasiliano na kuchochea maendeleo nchini. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel katika kituo cha Shirika la Reli Tanzania (SGR) jijini Dar es Salaam tarehe 7 Novemba 2024, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Eliud Sanga, amesema mradi wa SGR, ambao umepata mapato ya shilingi bilioni 15.6 tangu Juni 2024, unaonesha dhamira ya serikali kuboresha miundombinu ya Tanzania na kuunda fursa mpya za kiuchumi na maendeleo ya kijamii.

Sanga ameongeza kuwa Airtel imeingia ubia wa kibiashara na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kupitia vituo vya Treni za mwendo Kasi SGR  ili kuimarisha jitihada za kuwapa wananchi huduma za uhakika za kidigitali.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amesema ushirikiano huu utarahisisha upatikanaji wa huduma za tiketi na kifedha kupitia Airtel Money kwa wateja wa reli, na kuboresha huduma za mtandao wanapokuwa safarini.




Post a Comment

0 Comments