KAMPUNI YA MAWASILIANO YA TIGO YABADILISHA JINA KUWA YAS

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo imebadili jina na kuitwa Yas,huku huduma zake za kifedha, Tigo Pesa, zikibadilishwa kuwa Mixx by Yas


Mabadiliko hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Jerry Silaa


Rostam Azizi, Mwenyekiti wa Bodi ya Yas Tanzania, alisema;

“Yas ni ishara ya nguvu tuliyonayo Afrika. Mabadiliko haya yanaonesha dhamira yetu ya kuendelea kuwekeza na kuleta mageuzi ya kidijitali nchini Tanzania, bara na Visiwani. Tukishirikiana na Axian Telecom Group, tumejipanga kutengeneza fursa mpya, kuhamasisha ubunifu, na kujenga mustakabali bora ulio na lengo la kuimarisha sekta ya mawasiliano.”


Jerome Albou, Kaimu Afisa Mkuu wa Yas Tanzania, aliongeza:

“Leo ni siku ya kihistoria kwa kampuni yetu. Kama Yas, tumejipanga kuwa mshirika wa maendeleo, tukiwapa nguvu wateja wetu na kuwahakikishia kuwa biashara zitastawi katika mazingira yenye ushindani mkubwa.



Post a Comment

0 Comments