MWANAMITINDO Happiness Magese anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu kwenye tamasha la 'Samia Fashion Festival" linalotarajia kufanyika Novemba 30, 2024 Zanzibar.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 28, 2024 jijini Dar es Saam na Mwandaaji wa Tamasha hilo Hadija Mwanamboka.
"Huu ni mwandelezo wa Samia Fashion Festival, katika awamu ya kwanza Jaji Mkuu alikuwa ni Miriamu Odemba, na Kwa awamu hii ya Pili atakuwa ni Happiness Magese," amesema Mwanamboka.
Mwanamboka amesema lengo la Tamasha hili ni kukuza ubunifu na mitindo nchini samabamba na kuenzi vazi la Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Magese amesema ni heshima na furaha kwake kuwa Jaji Mkuu wa Tamasha hilo.
"Ninajivunia kushuhudia Wakati huu wa kihistoria, Wakati ambao tunasherehekea ubunifu, stara na urithi wa kipekee wa Rais Wetu wa Kwanza mwanamke, Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesema Magese.
Naye Idris Sultan ametoa rai kwa Watanzania kuunga mkono Wanawake wanaofanya kazi nzuri.


0 Comments