MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR ATUA KIBAHA KUWAHIMIZA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA KESHO



NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


 Makamu wa pili wa Rais wa  Zanzibar Hemed Abdulla amewahimiza wanachama wa CCM kuwa na upendo na umoja katika kushiriki kikamilifu kupiga kura na kuwachagua wagombea wote wa ccm  katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu nchi nzima.


Makamu huyo ameyasema hayo wakati wa halfa ya kufunga rasmi kampeni za uchaguzi za Mkoa wa Pwani ambazo ziimefanyika katika viwanja vya stendi ya zamani maili moja.


Makamu alisema kwamba wana ccm wanapaswa kutofanya makosa na kuhakikisha kwamba wanajitokeza kwa wingi na kuwachagua wagombea wote wa chama cha mapinduzi kwa asilimia 100.


Alisema kwamba ana imani kubwa Mkoa wa Pwani kwa kuwa uliweza kuongoza kitaifa  katika zoezi la uandikishaji katika daftari kwa ajili ya kupiga kura basi wajitahidi kushinda kwa kishindo katika mitaa yote kwa asilimi 100.


Katika hatua nyingine alitumia hotuba yake kumshukuru kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe:Silvestry Koka pamoja na wabunge wenzake wa Mkoa wa Pwani kwa kuweza kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo.


Makamu huyo wa pili wa Rais alisema kwamba amefarika kuona Mbunge Koka pamoja na wenzake wameweza kufanya kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo katika kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo.


"Nimesikia hotuba nzuri ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini amezungumzia mambo mbali mbali ikiwemo suala la changamoto ya huduma ya maji kwa wananchi wa Pangani na Viziwaziwa na mimi nimelichukua na nitamwambia Waziri Juma aweso kuhusiana na jambo hili ili wananchi waweze kupata huduma ya maji,"alisema Makamu wa pili.


 Aliongeza kuwa wanachama pamoja na wapinzani kutofanya vurugu za aina yoyote katika zoezi la upigaji kura na badala yake wapige kura kwa amani bila vurugu zozote.


 "Sisi atuna kinyongo kabisa na wapinzani kitu kikubwa ni kuwa na amani lakini katika kupiga kura wote tuhakikishe tunachagua wagombea wa chama cha mapinduzi kwa asilimia zote 100,"alisisitiza Makamu huyo.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe:Silvestry Koka alisema kwamba anamshukuru Rais Samia kwa kuweza kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa wananchi.


Koka alisema katika jimbo la kibaha mjini kuna miradi mbali mbali imetekelezwa katika sekta mbali mbali isipo kuwa ombi lake kubwa ni kumuomba Waziri wa maji Juma Aweso kutekeleza  ahadi yake ya maji katika Kata za Pangani na Viziwaziwa.


Naye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mwishehe Mlao alisema kwamba wamejipanga vilivyo katika uchaguzi huo na lengo lao ni kuibuka na  ushindi wa kishindo cha asilimia 100.


Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu nchi nzima ambapo kwa Mkoa wa Pwani hali ya ulinzi na usalama umeimarisha katika halmashauri zote tisa.


     






Post a Comment

0 Comments