RAS WA NDAKI YA SAYANSI ZA JAMII PROF CHRSTINE NOE WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) AHIMIZA WANASAYANSI KUPAZA SAUTI ZAO



Prof.Christine Noe,Ras wa ndaki ya sayansi za jamii wa Chuo kikuu cha dar es salaam(UDSM) katika kuhitimisha kilele cha kongamano la kimataifa la sauti ya sayansi za jamii,October 8 lillilofanyika Chuo kikuu cha dar es salaam alisema kuwa wanasayansi  za jamii wapaze sauti zao katika jamii ili kutatua matatizo yao ambapo alisema “Tumekubaliana kwamba turudi kwenye nafasi zetu kama wanataaluma na tuhakikishe kwamba tunapaza sauti za wanasayansi zifike kwa jamii na kwamba sauti zetu ni muhimu sana katika jamii ili kuleta tija katika taaluma,na ndivyo tutakavyoweza kufanya vyuo vyetu kuwa mahali ambapo maarifa yanatengenezwa”


Na aliongezea kuwa“Wito wangu utaenda sawa na sisi tunachokisimamia kwamba sauti za jamii zipo,sauti za wanasayansi zipo,sasa jamii inapaswa kusikiliza sauti za jamii kwa sababu jamii pia inamaarifa yake”alisema Prof.Noe 


Vilevile  alisema kuwa jamii na wanayansi za jamii zisikilizane ili kutatua matatizo“Tunasikiliza jamii pia jamii itusiikilize na tunatoa wito pia serikali  itusikilize,lakini tumeanza sisi wenyewe tuna jambo la kufanya ili kuwezesha jamii ya wanataaluma kuwa na sauti itakayosikilizwa jamii na itakayosikilizwa na seriakali”alisema Prof.Noe


Pia aliongezea kwa kusema kuwa “wanataluma, hii ni kawaida yetu ya kujadili matokeo ya taaluma yetu,pia mtegemee kwamba mijadala hii itaendelea,pia mijadala kwetu ni kama chakula,wanataaluma wanakula mijadala kutokana na tafiti zao na baada ya hapo wanaishauri serikali”alisema Prof.Noe

Post a Comment

0 Comments