WASOMI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM(UDSM)WAELEZA UMUHIMU WA VOICE OF SOCIAL SCIENCE INTERNATIONAL CONFERENECE(VSS2024)

 Wasomi waeleza umuhimu wa kongamano la kimataifa la sauti la sayansi lijulikanalo kama(8thVOICE OF SOCIAL SCIENCE INTERNATIONAL CONFERENCE(VSS2024) lilofanyika chuo kikuu cha Dar es salaam kuanzia tarehe 6 mpaka 8 october mwka huu ambapo Dkt samwel ntapanta kutoka Chuo kikuu  Denmark alisema kuwa

 "Nimeshiriki mjadala unaongelea athari za kemikali za mercury kwa wachimbaji wa madini,jinsi gani inaathiri afya zao,na moja ya mawasilisho yalikuwa jinsi gani hizi kemikali zinavyoathiri wanawake na zinavyosafirishwa kutoka kwa wanawake kwenda kwa watoto"aliongezea kwa kusema "lakini nilishiriki pia kwenye mjadala unaohusu uzalishaji wa kahawa Tanzania na mabadiliko ya tabia ya nchi,kama vile jinsi gani wananchi kule mbozi na maeneo mengine wanapambana na Mabadiliko ya tabia ya nchi,kama kuongezeka kwa joto,mvua zisizotabirika" alisema Dkt Ntapanta.

Pia Dkt JIA HUI LEE kutoka Chuo kikuu cha Bayreuth Ujerumani  alisema kuwa "Nimejifunza madhara ya kuchimba madini Tanzania na Kenya,hivyo ni muhimu sana kuheshimu utafiti ambao umetengenezwa na watafiti wa Tanzania na wa bara la Afrika kwa ujumla"





Naye Memory modest Njakile mwanafunzi wa shahada ya uzamili ya kutoka Chuo kikuu cha Dar es alam(Udsm)alisema kuwa" nilishiriki kwenye mada ya uwezeshaji wa teknolojia katika kuhakikisha masuala ya kujiunga na bima ya afya,Kama vile kupitia mitandao ya simu au namna yoyote ile ya teknolojia ambayo inarahisisha kujiunga badala ya kwanza ofisini kujiunga

Pia aliongezea kwa kusema "Mkutano huu umekuwa ni mzuri kwa sababu umeweza kukutanisha watafiti na watalaamu mbalimbali ambao wameongea mambo mbali ambayo yanaikumba jamii yetu kwa sasa,lakini pia mkutano huu umeweza kusaidia kubadilishana mawazo ya utafiti,NASA katika nchi zao na kwa nchi yetu ambapo tumeona kwa pamoja tunaweza kutatua matatizo ya kisayansi hasa kupitia Tafiti" alisema Njakile

Post a Comment

0 Comments