Na Francisco Peter , Dar es Salaam
Shirika la Bima la Taifa (NIC) imetiliana Saini ya makubaliano (MOU) kati yake na Benki ya Equity Tanzania yenye lengo la
kumlinda mteja na majanga mbalimbali na kuwa na uhakika wa mali zao na bidhaa zao kulindwa.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa NIC Kaimu Abdi Mkeyenge amesema huo ni mwanzo mwingine muhimu katika kufanikishawakulima watakaopata fedha kupitia equity watakuwa salama Kwa kukatiwa bima na NIC.
"(MOU) kati yetu na Benki ya Equity Tanzania ina lengo la kumlinda mteja na majanga mbalimbali na kuwa na uhakika wa mali zao na bidhaa zao kulindwa,"amesema Mkeyenge.
Amesema wameelekeza zaidi nguvu kwenye mikopo ya sekta ya Kilimo Ili kuhakikisha lengo lao la kushirikiana kwenye biashara ni kusukuma mbele uchumi kwenye sekta ya fedha.
" Tunataka kutumika katika kuiwezeshe Benki ya Equity kuwa na uwezo wa kukopesha na wao kutumika kama kampuni ya kukata bima kwenye mikopo ya wateja,"amesema Mkeyenge.
Mkeyenge aliongeza kuwa jukumu kubwa katika sekta ya bima ni lazima kushirikiana na benki za biashara Kwa kuwekeza kuchagiza ziwe na uwezo wa kukopesha watanzania kwa usalama Kwa mikopo hiyo kukatiwa bima.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Isabela Maganga amesema kuwa mashirikiano hayo ni ya kimkakati na NIC kwenye huduma wanazotoa zenye wateja wengi hususani Kilimo ili kuwezesha wateja kulindwa na majanga kupitia bima.
“Mpaka tunafunga mwaka 2024 wateja 20000 wamekopa Kwa njia ya digital sawa na asilimia 67 ambapo wateja wamechukua mikopo zaidi ya bilioni 300 ambayo tumetoa kupitia njia ya kidigitali” Amesema Bi.Isabela.
Aidha amesema, Mashirikiano yao na NIC yataleta tija kwenye sekta ya uchumi wa kifedha kutokana na utalaamu wa Bima walio nao NIC kwa ajili ya kumlinda mteja na majanga mbalimbali na kuwa na uhakika wa mali zao na bidhaa zao kulindwa.
Hivyo basi amesema malengo ya mwaka 2025 ni kuhakikisha kuwa wanafanya mara mbili ya mwaka 2024 kwa kuongeza wigo wa watumiaji wa bima na kuongeza elimu kwa umma kuhusu bima.

0 Comments