Airtel Africa kwa ushirikiano na SpaceX wametangaza kufanikiwa kwa majaribio ya huduma za data na ujumbe (SMS) kupitia Starlink Mobile nchini Kenya, hatua muhimu inayofungua njia ya kuleta mawasiliano ya satelaiti moja kwa moja kwenye simu za mkononi kwa mamilioni ya wananchi katika nchi 14 ambako Airtel inafanya kazi barani Afrika.
Majiribio hayo yalifanyika katika maeneo yasiyokuwa na mtandao wa kawaida wa simu, yanayojulikana kama maeneo ambayo minara ya mawasiliano ya ardhini haikuwepo na mawimbi. Katika maeneo hayo, huduma ya Starlink Mobile iliwezesha moja kwa moja na kuruhusu simu za mkononi zinazotumia teknolojia ya 4G kuunganishwa na mtandao wa satelaiti zaidi ya kilomita 650 zilizo juu angani, hivyo kuwezesha watumiaji kuendelea kuwa na mawasiliano hata katika maeneo ya mbali kabisa.
Katika kipindi cha majaribio, huduma hiyo iliweza kusaidia matumizi ya data nyepesi kama vile kupiga na kutuma ujumbe kupitia WhatsApp, kutumia ramani, Facebook Messenger pamoja na kufungua mialiko ya kifedha kupitia programu ya Airtel App. Watumiaji waliweza kuendelea kutumia huduma muhimu hata walipokuwa katika maeneo ambayo kwa kawaida hayana mtandao wa simu.
Akizungumzia mafanikio hayo, Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa, Sunil Taldar, alisema hatua hiyo inaonesha utekelezaji wa vitendo baada ya tangazo la ushirikiano kati ya Airtel Africa na SpaceX. Alisema majaribio yaliyofanyika nchini Kenya yanaonesha dhamira ya kampuni hiyo kupanua upatikanaji wa mawasiliano kwa watu wengi zaidi barani Afrika.
Aliongeza kuwa kwa kuunganisha teknolojia ya Starlink Mobile, Airtel Africa ina hakikisha wateja wake wanaendelea kuwa na mawasiliano hata wanaposafiri nje ya maeneo yenye mtandao wa kawaida wa simu.
Baada ya majaribio hayo nchini Kenya, Airtel Africa na Starlink Mobile wanatarajia kutumia uzoefu walioupata kupanua huduma hiyo katika nchi zote 14 ambako Airtel inafanya kazi, kulingana na vibali vya mamlaka za mawasiliano kwa kila nchi.
Aidha, kampuni hizo zinapanga kuanzisha huduma za kupiga simu kwa sauti pamoja na huduma za zenye uwezo mkubwa zaidi kupitia teknolojia ya Starlink Mobile V2, ambayo itawezesha watumiaji kupata huduma ya intaneti ya kasi moja kwa moja kwenye simu zao bila kutegemea minara ya kawaida ya mawasiliano.

0 Comments