Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu hii leo ameshuhudia ujazaji maji bwawa la Umeme la Nyerere Lililopo Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.
Samia ameielekeza Wizara ya Uvuvi na Mifugo kuweka mpango mahsusi wa ufugaji wa kisasa wa samaki katika bwawa la Nyerere.
Amesema kwa kuwa bwawa hilo lipo ndani ya hifadhi, uvuvi utakaofanyika hapo ni lazima uwewe wa kisasa na wa mfano.
“Kupitia bwawa hili tumejenga daraja kubwa na bora zaidi kuiunganisha mikoa ya kusini, kilichobakia sasa ni barabara. Nielekeze Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi hasa TANROADS, kuandaa mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Chalinze hadi Utete kupitia kwenye dara hilo.“ Rais Dkt Samia Suluhu.
Njia hiyo itafupisha sana usafiri kati ya mikoa ya kusini na kaskazini mwa Tanzania.
“Bwawa hili litaweza kuweka akiba kubwa ya maji na kuzalisha umeme hata pale mvua inapokuwa imepungua. Litatusaidia pia kudhibiti mafuriko ya mara kwa mara ya mto Rufiji na kuwezesha kilimo cha uhakika cha umwagiliaji maji” Rais Dkt Samia Suluhu.
“Sote katika umoja wetu tunapaswa kujivunia na kudhihirisha umoja, utaifa na uzalendo wetu, kwa kuendeleza na kuulinda mradi huu muhimu kwa maendeleo yetu. Na kwa muktadha huo nazidi kuwakumbusha kuwa mradi huu ni fahari ya nchi yetu na tunautekeleza kwa gharama kubwa na kwa jasho la kila Mtanzania kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo” Rais Dkt Samia Suluhu
0 Comments