KONGAMANO LA HUSTLESASA KUFANYIKA AGOST 15 LUGALO GOLF CLUB
MOSSES BLISS KUTUMBUIZA KWENYE TAMASHA LA MUZIKI WA INJILI AGOST 15 DAR
HUSTLESASA, kongamano linalolenga kuwaunganisha vijana kupitia muziki, burudani, biashara na imani, maandalizi yanaendelea kwa kasi kuelekea tukio hilo litakalofanyika Agosti 15 katika Lugalo Golf Club.
Kongamano hilo litakuwa na shughuli mbalimbali pamoja na fursa za biashara, huku likilenga pia kuibua jambo jipya na kuwapa vijana nafasi ya kukutana, kushirikiana na kujenga jamii yenye maono mapya.
Miongoni mwa wageni muhimu atakayeshiriki ni Moses Bliss, muimbaji maarufu kutoka Nigeria, ambaye atashiriki katika muda maalum wa ibada, maombi na ushuhuda.
Waandaaji wamesema tukio hilo halilengi burudani pekee, bali pia kuwawezesha vijana kuelewa umuhimu wa kuishi katika Kristo, kujenga imani na kushirikiana katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Aidha, NEEMA Gospel Choir pamoja na baadhi ya wacheza dansi watashiriki katika kongamano hilo, huku kukiwa na vipengele mbalimbali vya muziki na burudani.
Waandaaji pia wametaja Seed Communion kama sehemu ya programu ya siku hiyo, wakisisitiza kuwa washiriki hawatarajiwi kuja kujiburudisha pekee, bali pia kushiriki katika kujenga jamii yao.
“Sio kwamba mnakuja kuinjoy tu, ila mnatakiwa kuijenga jamii yenu.”
HUSTLESASA inatarajiwa kuwa wakati wa kuadhimisha mwanzo mpya, kuunganisha vijana na kuwapa nafasi ya kushirikiana kupitia muziki, imani, biashara na vipaji.
0 Comments