Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Mgore Miraji Kigera, amefika Kizimkazi, Zanzibar, kutoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.
Mgore Kigera amefika Kizimkazi akiwa pamoja na wabunge wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa ajili ya kuungana na Rais Samia pamoja na familia yake katika kipindi hiki cha majonzi.
Katika ziara hiyo, Mbunge huyo ametoa salamu za pole na faraja kwa Rais Samia, huku akionesha mshikamano na familia katika kipindi hiki cha msiba.
Ujio wa viongozi hao Kizimkazi ni sehemu ya kuungana na familia ya Rais Samia katika kipindi cha maombolezo na kutoa faraja kufuatia kuondokewa na mpendwa wa

0 Comments