WANAFUNZI 150 KUPATA UFADHILI WA MASOMO ALGERIA KUPITIA SAMIA SCHOLARSHIP

Serikali imetangaza nafasi 150 za wanafunzi wa Kitanzania waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi kupata ufadhili wa masomo nchini Algeria kupitia mpango wa Samia Scholarship.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema wanafunzi hao watachaguliwa miongoni mwa wanafunzi 1,000 waliopata Samia Scholarship ya STEM ya kusoma katika vyuo vya ndani, kwa kuzingatia ufaulu wao katika masomo ya sayansi bila kujali uwezo wa kifedha wa familia zao.

Amesema Serikali ya Algeria itagharamia ada za masomo, huku Serikali ya Tanzania kupitia Samia Scholarship ikigharamia mahitaji ya maisha ya wanafunzi hao watakapokuwa nchini humo.

Wanafunzi hao pia watahitajika kujiandaa kujifunza lugha ya Kifaransa, huku fursa hiyo ikilenga kuwawezesha kupata ujuzi katika maeneo muhimu kama sayansi ya data, akili bandia (AI), machine learning, teknolojia ya habari, uhandisi na tiba.



#MzalendoTVUpdates

Post a Comment

0 Comments