Na Sheila Ahmadi
Mamlaka ya Usimamizi wa bandari TPA imepokea meli kubwa ya watalii aina ya Norwegian Dawn yenye urefu wa mita 294 huku i kipitia bandari tofauti tofauti ikiwemo bandari ya mombasa hadi kufika nchini Tanzania ambapo uwezo wa meli hiyo ni kubwa inaweza kubeba abiria 4000 ambapo baadhi ya watalii waliosafiri na meli hiyo ni 2400 kuja nchini Tanzania.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa bandari ya Dar es salam Mrisho mrisho mara baada ya mapokezi ya meli hiyo ambapo amesema kuwa watalii ambao wamefika kwenye meli hiyo ni zaidi ya 2210 huku baadhi ya wengine wakiwemo wafanyakazi wa meli hiyo ni 1000 hivyo meli hiyo ina ukubwa wa hali ya juu.
Ukubwa wa meli hiyo ina urefu wa kina 294 hivyo kupitia Royal tour imezaa matunda na imeweza kuleta watalii mbalimbali kutoka nchi Za nje kuja Tanzania kutembelea vivutio vya watalii ikiwemo mbuga ya selou, Fukwe za bahari, na makumbusho yaliyopo jijini dar es salaam.
" Sisi kama bandari Tunafurahi kama ambavyo wao wenyewe wamefurahi kuja kutembea nchini Tanzania kwa huduma ambazo wamezipata bandarini kwa kushirikiana na kapteni ambaye amehusika kupokea meli hiyo na kuweza kuhakikisha usalama unaimarika kwa watalii hao.
Meli hiyo ikitoka bandari ya dar es salaam itaelekea Msumbiji kwenye bandari nyingine huku dare salaam ikiweza kukaa kwa mda mchache huku ulinzi na usalama ukiwezeshwa kwenye maeneo yote ya bandari hiyo ili watalii hao waweze kufanya utalii ulio bora zaidi
Kwa bandari ya Dar es salaam ni mara ya kwanza kuweza kupokea meli kubwa na yenye urefu wa kina kirefu hivyo mamlaka ya bandari inajivunia kuweka maboresho ambayo yanafanywa katika bandari hiyo na kuweka mlango ambao meli hiyo imepitishwa hivyo matarajio yetu ni kuweza kuhudumia meli zenye urefu wa mita 305. "Amesema mkurugenzi Mrisho"
Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za meli kutoka bandari zote nchini zikiwemo bandari ya Tanga Mtwara, na Dar es salaam Ndugu Mwengamno amesema meli hiyo inahudumia mizigo na abiria ambapo mamlaka ya bandari Tanzania TPA kwa kushirikiana na menejimeti imeweza kuboresha bandari kwa kiasi cha kuweza kupokea meli zenye kina kirefu.
Kwa kushirikiana na waongozaji wa meli nchini wameweza kuweka mazingira wezeshi ya kupokea bidhaa kutoka kwenye meli na bidhaa mbalimbali yakiwemo magari na rasilimali za watu hivyo bandari ya dar esa laam, Tanga na mtwara yatakua na ushindani wa kibiashara.




0 Comments