MAMLAKA ya Uhifadhi wa Ngorongoro imetangaza kuongeza kasi ya kuwahamidha wananchi wanaoishi katika hifadhi ya Ngorongoro kutokana na nyumba zako zinazojengwa eneo la Msomera Mipango Tanga kukamilika.
Pia imewahakikishia watanzania kuwa hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu katika zoezi linaloendelea la kuwahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa hiari na kuwapeleka maeneo yaliyotengwa.
Akitoa taarifa hiyo Ofisa Mfawidhi Mwandamizi Uhusiano wa Umma,Kassim Nyaki wakati akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea hifadhi hiyo alisema hadi kufikia Machi mwaka huu wanatarajia kuhakisha Jaya 20000.
“Kaya 10000 zitahamia Msomera, Kitwai(Simanjiro) na Saints, kaya 4000zitahamia maeneo mengine ambayo wananchi watayachagua wenyewe na 6000 zitahama baada ya marekebisho ya sheria,”alisema.
Alitalia mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi kifupi cha maradi kuwa ni wananchi waliohamia Msomera wanajishughulisha na kilimo na kijipatia Chakula, Wananchi waliohamia kujengewa nyumba zaidi ya walizokabidhiwa na Serikali.
Pia maeneo yaliyokuwa yanakaliwa na watu Miguel imeanza kurudi na msukumo wa viongozi wa Serikali katika kutekeleza maradi huo ni Mkubwa.
Vilevile alitaja wanayokabiliana nayo katika utekelezaji wa maradi kuwa ni kuwepo na idadi ndogo ya watumishi kutoa huduma kwa Jamii inayohamia Msomera kama walimu, Maofisa maendeleo ya jamii, mifugo.
Akizungumza jana Kamishna msaidizi wa uhifadhi Mipango ufuatiliaji na Tathmini kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Lilian Magoma,wakati akizungumza na waandish wa Habari kwenye ziara ya Waandishi wa habari walipoenda kutazama shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika Hifadhi ya Ngorongoro ambazo zinatajwa kuhalibu ustawi wa uhifadhi hiyo.
"Baadhi ya watu toka nje wanatumia vyombo vya habari kusemj kunaukiukwaji wa haki za binadamu jambo ambalo sio kweli ,katika utelekezaji wa zoezi hili hakuna jambo ilo kwani tumezingatia sheria na utu katika kuwahamisha"Amesema Magoma.
Magoma,amesema serikali imeingia katika Ghalama kubwa ya kuwalipa fidia,kuwasafirisha mali zao na kuwapa motisha ya milioni kumi,
Hata hivyo,Magoma ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa ngorongoro kuhama sehemu hiyo kwani kuna faida kubwa ikiwemo kulinda Hifadhi hiyo.



0 Comments