VYAMA 13 VYA UPINZANI VYATOA RAI KWA CHADEMA KUELEKEA MAANDAMANO 24 JANUARY



Na Sheila  Ahmadi


UMOJA wa Vyama 13 vya upinzani umekemea maandamano yaliyoandaliwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaliyopangwa kufanyika Januari 24 mwaka huu.


Miongoni mwa vyama vinavyounda umoja huo ni pamoja na Chama cha Democratic Party (DP), National Recontructio Alliance (NRA), United People's Democratic Party (UDPD), Alliance For Democratic Change (ADC), Demokrasia Makini, National League For Democracy (NLD), Tanzania Labour Party (TLP), Chama Cha SAU, Chama cha UD, CCK, AFD na ADA TADEA.


Tamko hilo  limetolewa kwa waandishi wa habari Jijini  Dar  es alaam   na  Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha DP Abdul Mluya amesema kitendo cha CHADEMA kuitisha maandamano ni kiashiria cha kutaka kuleta uvunjifu wa amani nchini.


"Tarehe 13 mwaka huu Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alitangaza maandamano kwa lengo la kupinga miswada mitatu iliyopelekwa bungeni kuhusuana na mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa, sisi vyama 13 hatukubaliani na hili wenzetu ambalo wameliamua," amesema Mluya.


Amesema kuwa njia hiyo ni kinyume na utaratibu kwani inakinzana na amani na umoja wa nchi na kwamba njia hiyo ni kiashiria cha kutaka kuleta uvunjifu wa amani. Mluya ameendelea kueleza kuwa hatua hiyo ya CHADEMA inaashiria ubinafsi mkubwa wanalionao na kujiona kwamba wao ni maalum na wanaweza kufanya jambo lolote wanalotaka.


Mluya amebeinisha kuwa chama hicho kimekuwa mara nyingi kikiwa kinyume na vyama vingine ambapo ameeleza kuwa mikutano mingi ya vyama vya siasa ambayo imekuwa ikifanyika kwa maslahi mapana ya Taifa chenyewe kimekuwa hakishiriki jambo ambalo hata malalamiko yao yanakuwa hayana msingi kwani wangetumia mikutano hiyo wanayokataa kushiriki kwa kutoa maoni yao.


Hivyo amekitaka Chama cha CHADEMA kufanya siasa za hoja badala ya kukimbilia kufanya maandamano kwa kuingiza wananchi barabarani.

Kwa upande wake  mpinzani kutoka chama cha ADC Doyo Hassan Doyo amesema kuwa   maandamano hayo ya CHADEMA yanaajenda ya siri, na kwamba kama moja ya ajenda inayosukuma maandamano hayo ni ugumu wa maisha, wao kama CHADEMA wanapaswa kuja na mbinu mbadala ya kusaidia wananchi waweze kuimarika kimaisha.





Post a Comment

0 Comments