Na Sheila Ahmadi
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema vifo vitokanavyo na mama wajawazito vimepungua kufikia hadi % 85 kwa mwaka 2023 ambapo serikali imeweza kutoa huduma za afya huku maeneo 15 nchini zikiwemo hosptali, Zahanati, na Vituo vya Afya.
Akizungumza Jijini Dar es salaam waziri wa afya Ummy Mwalimu mara baada ya kutoa Taarifa ya utoaji wa huduma za Afya kwa 2023 ambapo wizara hiyo imeweza kutoa huduma nchini kote Mjini na Vijijini lakini huduma zitolewazo mjini ni tofauti na kijijini tunaamini kuwa ongezeko la jitihada za watumishi zinaenda kuboreshwa mwaka huu.
Huduma za afya kwa mama na Mtoto imeboeeshwa zaidi katika mwaka uliopita ambapo wajawazito asilimia 97 wamehudhuria kiliniki katika kuweza kupata huduma mara nne katika kipindi cha ujauzito kwani ni muhimu kwa wajawazito katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
" Hatujafikia malengo madhubuti kwani vifo vya akina mama wajawazito vilikua 556 2023 kutoka elfu 11 kwa Mwaka na kuweza kuzuia vifo hivyo na upasuaji wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni kwa huku wanawake asilimia mbili wamejifungua kwa njia ya upasuaji "Amesema UMmy Mwalimu.
Tanzania imekuwa kimbilio kwa Matibabu mbalimbai ya magonjwa kwani wageni kutoka nje ya nchi wanakuja kutibiwa nchini humo zikiwemo nchi ya Malawi, Zambia, Na Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo hivyo Fedha za kigeni hupatikana kupitia Wizara ya afya.
Ametoa pongezi kwa Watumishi wa afya Mkoa wa kagera kwa kuweza kushirikiana na serikali katika kuhudumia watu wenye ugonjwa wa Murbug ambao ulitokea mwaka jana mkoani Kagera huku baadhi ya magonjwa mbalimbali yakiwemo Mafua, Malaria, na ukimwi vimepungua.
Mwaka huu 20224 wizara ya afya kwa kushirikiana na serikali kwenda kuboresha huduma za afya na kupunguza magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza.
Waziri ummy ametoa wito kwa wananchi kuacha kutumia vitu vyenye sukari, nyingi na chumvi hivyo wananchi ni vyema kuwasikiliza watu wenye Dhamana ya Afya akiwemo Dkt Janabi ambaye anahamasisha afya.

0 Comments