The Foundation For Tomorrow laendelea kutoa Udhamini kwa wanafunzi na Mafunzo ya Walimu




Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na utoaji wa elimu Bora kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu la The Foundation For Tomorrow limesema linaendelea na Programu ya kusaidia udhamini wa masomo kwa watoto kuanzia Ngazi ya elimu ya awali hadi Kidato cha Sita ili waweze kujikwamua kimaisha na kutimiza malengo yao.


Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa shirika hilo Thabisani Ncube  katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Ubora wa Elimu ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).

 Amesema  kuwa shirika hilo jukumu la kuhakikisha  jamii inajua kusoma na kuandika hivyo wanatoa udhamini na mahitaji mwingine muhimu kwa watoto hai.





              Mkurugenzi wa The Foundation For Tomorrow,Thabisani Ncube akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salam katika Mkutano Pili wa Kimataifa wa Ubora wa Elimu ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).


" Tuna mpaka 15 katika ufanyaji kazi tunakikisha watu wanajua kusoma na kuandika kwa kuwaza elimu bora," amesema Ncube.

Amebainisha Kuwa Wana program ya kutoa mafunzo kwa walimu waliopo makazini na kwamba wanatoa kuwajengea uwezo watoe elimu bora kwa wanafunzi.

Amesisitiza kuwa mbali na udhamini huo wanatoa chakula kwa wanafunzi shuleni ili kuwasaidia kufuatilia vyema masomo na kupata ufaulu wa juu.

Ameongeza kuwa kuna shule sita eneo la Umasaini wanatoa huduma ya chakula kwa wanafunzi.
 
Kwa upande wake, Meneja wa Programu ya Mafunzo kwa Walimu wa The Foundation For Tomorrow, Noah Kayanda amesema kuwa Wana Programu ya mafunzo kwa viongozi wa shule hivyo wanatoa ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo kiutendaji. 


Meneja wa Programu ya Mafunzo kwa Walimu wa The Foundation  For Tomorrow, Noah Kayanda akizungumza na wanahabari leo jijini humo katika banda la shirika hilo kwenye Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Ubora wa Elimu ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET



.

Post a Comment

0 Comments