UZALALISHAJI CHANZO CHA MAJI MTO RUVU WAPUNGUA KWA ASILIMIA 64 KUTOKANA NA UKAME.



Na Mwandishi Wetu.

Serikali imesema kwamba kwa sasa hali ya kiwango cha uzalishaji wa  maji katika mto Ruvu  kimepungua kwa asilimia 64  kutokana na kuwepo kwa changamoto kubwa  ukosefu wa mvua za vuli uliosabishwa na madaliko ya tabia ya nchi na kupelekea kuwepo kwa ukame.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makala wakati wa ziara ya bodi ya wakurugenzi wa Dawasa , pamoja Kamati ya ulinzi na usalama ya Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea hali halisi ya kupungua kwa kiwango cha maji.
 


Aidha mkuu  huyo akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa ya Pwani na Morogoro amesema kwamba jitihada za serikali katika kuhakikisha maji yaliyopo yanawafikia wananchi japo kwa mgao hadi hapo mvua zitakaponyesha.


Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na bodi ya wakurugenzi wa dawasa wamefanya ziara hiyo katika mitambo ya ruvu chini pamoja na ruvu chini ambapo wamebaini kuwepo kwa kiwango cha maji kupungua. 



                        

Post a Comment

0 Comments