MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA VIVUKO VITATU Mkuu wa mkoa wa

  






Mwanza Adam Malima amefanya uzinduzi wa vivuko vipya vitatu kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo ya Nyakaliro - Kome,Bwiru - Bukondo na Ijinga - Kahangala ili kuondoa kero za usafiri kwa wananchi na kuwaletea maisha bora huku akiitaka kampuni ya kizaendo ya Songoro Marine Transport kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na viwango vya hali ya juu


Aidha kipekee kabisa naishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huu mkubwa katika kuondoa kero ya usafiri kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza na watanzania kwa ujumla Uwekezaji huu utainua hali za kiuchumi na kijamii zitakazonufaika, Adam Malima Mkuu wa mkoa wa Mwanza


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ( Sekta ya Ujenzi )Ludovick Nduhiye, amesema uzinduzi vivuko vitatu ambavyo vimezinduliwa vimekuwa hitaji kubwa kwa wananchi wanaoishi maeneo ambayo vivuko hivyo vitaenda kutoa huduma baada ya ujenzi wake kukamilika


Ni mategemeo ya Wizara kuwa wananchi katika maeneo husika watatumia fursa hii ya kuimarisha kwa usafiri kuimarisha shughuli zao za kiuchumi ili kufikia azma ya Serikali yetu ya kuwaletea maendeleo wananchi, Lidovick Nduhiye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ( Sekta ya Ujenzi )


Ni mategemeo ya Wizara kuwa wananchi katika maeneo husika watatumia fursa hii ya kuimarisha kwa usafiri kuimarisha shughuli zao za kiuchumi ili kufikia azma ya Serikali yetu ya kuwaletea maendeleo wananchi, Lidovick Nduhiye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ( Sekta ya Ujenzi )


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na  Umeme Tanzania  ( TEMESA ) Lazaro kilahala amesema ujenzi wa vivuko vitatu unaofanywa na Kampuni ya Songoro Marine Transport ambayo ndiyo ilishinda zabuni ya kazi hiyo umegharimu kiasi cha gharama zaidi ya shilingi bilioni 15 


Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Major Songoro amesema, vivuko vyote vitatu vinajengwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa  ( IMO ) na kitaifa ( TASAC ) huku akisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha vivuko hivyo vinakamilika katika muda uliopangwa yaani mwezi Julai 2023 kama walivyokubaliana na Temesa.

Post a Comment

0 Comments