Wananchi wa Kata ya Marangu Magharibi Kijiji cha Komela Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro wameingia katika taharuki baada ya Mtuhumiwa, Shukuru Nguma (20) kukiri kufanya ukatili kwa kulawiti watoto 18 kijijini hapo na vijiji jirani.
Inaelezwa kuwa Mtuhumiwa huyo alikiri kufanya kitendo hicho kwa watoto wa familia aliyo kuwa anaishi nao pamoja na watoto wengine kijiji hapo na vijiji jirani wote wakiwa ni Wanafunzi wa shule ya Msingi kwa nyakati tofauti.
Akizungumzia tukio hilo moja ya mzazi ambaye watoto wake watatu (3) wamefanyiwa ukatili huo ameeleza kuwa aliitwa shuleni baada ya watoto kupewa elimu ya matukio ya ukatili na vitendo viovu ndipo mtoto mmoja alipo nyosha kidole na kukiri kuwahi kufanyiwa kitendo cha ulawiti na Kijana huyo huku akiwarubuni kwa kuwapa pipi na pesa.
"Walimu walibaini hilo wakati wakiwa mstarini (parade) na alipo ulizwa kulikoni alisema kuwa huyo Shukuru amemfanyia kitendo cha ulawiti na kumtaka asiseme kwani ataendelea kumpa zawadi na ikiwa atasema basi atamfanya kitu kibaya ambapo alitaja na watoto wenzake walio wahi kufanyiwa kitendo hicho cha kinyama." alieza Mama wa mhanga.
Baba wa mtoto mwingine aliye fanyiwa ukatili wa kulawitiwa naye alieleza kuwa amekuwa karibu na mtoto wake wa kiume ila hajawahi mweleza changamoto anayopitia jambo linalo mshangaza ni mbinu gani ya kitisha mtuhumiwa amekuwa akiitoa kwa watoto anaowafanyia ukatili.
"Yaani siyo kuwa sipo karibu na familia yangu hapana,nipo nayo karibu na nirafiki kwa watoto wangu ila nashangaa tukio hili ameshindwa kuniambia inaelekea wanapewa kitisho kikubwa sana,sijawahi muona akitembea kwa shida useme ningeshtukia mchezo huo bado nashangaa kama mzazi"alieleza.
Akizungumzia tukio hilo moja ya Mwalimu ambaye hakutaka kutaja jina lake ameeleza kuwa watoto walio fanyiwa kitendo hicho kwa shule aliyopo ni sita (6) huku wengine wakitoka katika Vijiji vingine ikiwemo,Mbahe ,Arisi na Lyasongoro kutokana Mtuhumiwa kutaja watoto hao.
"Huwa tuna utaratibu waa kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili kwa Watoto,sasa tulikuwa mstarini (Parade) na elimu ya athari ya vitendo vya ukatili ikiwemo ulawiti ilitolewa ndipo mtoto mmoja (jina limehifadhiwa) alipo nyooshaa kidole ma kueleza kuwahi kufanyiwa kitendo hicho na kutaja wenzake"
Aliongeza kusema kuwa," baada ya kutaja wenzake tuliwahoji nao wakakiri na kumtaja kijana aliyekuwa akifanya kitendo hicho kuwa ni Shukuru Nguma,tulipo pata maelezo hayo ndipo tukaanza kutoa taarifa kwa ngazi mbalimbali." alieleza Mwalimu huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Cha Komela Anold Mtui amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa baada ya mtuhumiwa kukamatwa siku ya Jumamosi Januari 21.2023 alikiri mwenyewe kufanya kitendo cha kulawiti watoto 18 kwa kuwa taja majina yao na wazazi wao.
"Huyo mtuhumiwa siyo mara yake ya kwanza,aliwahi kutuhumiwa kwa vitendo hivyo miaka iliyo pita na alifungwa Magereza kisha akaachiliwa,tulipo pata hizi taarifa tulimsaka na alitoroka Kijiji hapa na kwenda huko Kijiji cha Mamba Kokire ila tulifanikiwa kumkamata"alisema Mtui
Mtui anaeleza kuwa walidhani kafanya ukatili kwa watoto wachache ila idadi iliongezeka kwa yeye kutaja watoto wengi zaidi na watoto walikiri kweli kufanyiwa.
"Alitaja mwenyewe hadi idadi ikafika 18 kati yao Msichana ni mmoja na huyo alimfanyia kitendo hicho kinyume na maumbile,hii inashangaza sana na kuogopesha wazazi waamke katika usingizi wafanye malezi kwa watoto wao vizuri kwa ukaribu" alieleza Mtui
Mkuu wa Wilaya hiyo Abbas Kayanda amekiri uwepo wa tukio hilo na kusema kuwa tayari mamlaka za uchunguzi zinaendelea kuchukua taarifa na mtuhumiwa bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi .
"Mtuhumiwa alikamatwa na alikiri kufanya vitendo hivyo,kipindi cha nyuma akiwa na miaka 17 aliwahi kufungwa kifungo cha nje kwa kufanya makosa kama hayo,sasa karudia tena, Polisi wanamalizia taratibu zinazotakiwa apandishwe Mahakamani" alisema Kayanda.
Kayanda ameeleza kuwa serikali haitawavumilia watu wanaofanya vitendo na tabia za namna hiyo katika Jamii badala yake itawakamata na kuwachukulia sheria na adhabu kali huku akiitaka Jamii kufichua vitendo vyote vya ukatili vinavyo fanywa kwa siri na ndugu wa karibu au mtu yeyote ambaye ana nia ovu ya kusababisha madhara kwa wengine hasa watoto wadogo.

0 Comments