Na mwandishi wetu Shinyanga
Watu wawili wamenusurika kupoteza maisha katika eneo la ushirika lililopo Mkoani Shinyanga baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah kupata ajali baada ya kuhama njia.
Mwandishi wa habari hizi ambaye aliweza kufika eneo hilo la tukio na kushuhudia gari hiyo ikiwa imehama njia na kutumbukia kwenye mtaro ambapo hata hivyo hakuna mtu yoyote ambaye amefariki dunia.
Katika tukio hilo kwenye gari walikuwa wamepanda watu wawili ambao inadaiwa kuwa ni mke na mume ambapo kutoka na ajali hiyo wamepata majeraha katika baadhi ya mikono na sehemu nyingine za mwili.
Baadhi ya mashuhuda ambao walishuhudia ajali hiyo wakizungumza na mwandishi wa habari hizi walisema kwamba chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari hiyo kutaka kulikwepa gari lingine upande wa kushoto ndipo gari hiyo ilipohama njia na kugonga nguzo za umeme na kutumbukia kwenye mtaro.
MWISHO.

0 Comments