KAMPUNI YA MAHINDRA NA GF TRUCK WAANZA KUZALISHA MAGARI NCHINI.

 

Na: Sheila Ahamadi


KAMPUNI ya Mahindra kutoka India kwa ubia na kampuni ya GF Truck wanatarajia kuanza uzalishaji na uuzaji wa magari hapa nchini.

Hayo yamesemwa jijini  dar  es salaam   na Waziri wa Nchi, Ofisi ya  Rais  Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo katika hafla ya uzinduzi wa uwepo Kampuni ya Mahindra nchini sambamba na uzinduzi wa magari yalizalishwa na Kampuni hukwa ushirikiano na GF Truck.


Prof. Mkumbo amesema  kuwa uzalishaji huo  wa magari hayo nchini inatarajia kuanza miezi sita ijayo kuanzia hivi sasa.


Aidha   Waziri Prof. Mkumbo amesema kutokana na Kampuni kuzalisha magari nchini, Serikali ina mpango kuifanyia marekebisho sheria ya uagizaji magari nchini ambayo inaruhusu hadi magari chakavu kuingia nchini ili kuzuia magari hayo na kulinda maslahi ya Viwanda  vya utengenezaji magari nchini.


Waziri Prof. Mkumbo amesisitiza kwa kusema kuwa   kwa sasa hapa nchini kumekuwa na viwanda vinavyotengeneza magari hivyo ni wakati wa kubadilisha sheria ya uigizaji magari.


"Sheria ya sasa inaruhusu mpaka magari chakavu yaingie nchini hivyo sheria tutaibadilishe ili kulinda viwanda hivi vinavyozalisha magari hapa nchini,” amesema Prof. Mkumbo.


Sambamba na hayo   Prof. Mkumbo amesema ujio wa kampuni ya Mahindra ni matokeo ya ziara ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini India mwezi Oktoba mwaka huu ambapo alikutana na kuzungumza na wawekezaji mbalimbali.


"Haya ni matunda ya ziara ya Rais Samia nchini India imepelekea ujio wa Kampuni hii kikubwa kuja kuwekeza hapa nchini,” ameongeza l.

Naye  , Mkurugenzi Mtendaji  kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), G ilead Teri, amesema kwa sasa hali ya uwekezaji Tanzania ni nzuri huku akiwataka Watanzania kujitokeza kwenye uwekezaji kwa kushirikiana wa wageni kutoka nje.








"Kama wewe Mtanzania unakiwanja, nyumba, shule, kiwanda na unataka ubia na mwekezaji njoo kwetu sisi tutakutafutia uwekezaji na mbia,” amesema Teri.


Kwa upande  wake  Mkurugenzi Mtendaji wa GF Group, Iman Karmali, amesema wapo nchini kwa miaka 17 na wameweza na kutoa ajira kwa watanzania nchini huku kampuni hiyo wakizalisha magari madogo

Post a Comment

0 Comments