Wafanyabiashara waaswa kuwa na TIN na leseni ili kulipa kodi stahiki zinazoendana na biashara zao kwa wakati kwa lengo la kuepukana na kodi enevu.
Amezungumza hayo mapema leo Februali 15, 2025 Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Biashara Mkoa wa Dar es Salaam Yusuph Yenga wakati wa ziara maalumu ya kuwatembelea wafanyabiashara eneo la Mbagala.
Amewashauri wafanyabiashara ambao hawajajiunga na jumuiya ya wafanyabiashara kujiunga ili kutatua changamoto zinazowakumbuka wafanyabiashara hao.
“Wafanyabiashara tunapaswa kulipa kodi stahiki ili kukuza uchumi wa nchi na kuepukana na kero zinazohusisha jambo hilo,”alisema
Alisema kuwa ziara hiyo itaenda mwezi mzima katika maeneo tofauti tofauti na amewaomba wafanyabiashara kudhuria mikutano hiyo ili kupata suluhu kwenye biashara zao.





0 Comments