Na Sheila Ahmadi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert chalamila ametembelea katika ofisi za mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya ambapo ametoa rai kwa wamiliki wa vijiwe hivyo ambapo vinatumika kwa matumizi ya dawa hizo na kwenda kupelekea Athari mbalimbali kwa watumiaji .
Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salam RC Chalamila alipotembelea kwenye ofisi hizo za udhibiti wa madawa ya kulevya ( DCEA) amesema serikali itaendelea kushirikiana na mamlaka hiyo ili kwenda kutokomeza wahalifu ambao wanatumia madawa hayo kwani yanaenda kupelekea changamoto ya Afya na Akili hususani mkoa wa Dar es salam.
Amesema wahalifu wengi kutoka mkoani humo wanaweka makazi na vijiwe kwenye maeneo ambayo ni hatarishi ikiwemo Eneo la Pemba mnazi kigamboni wahalifu hutumia eneo hilo kama kijiwe na kwa matumizi ya madawa.
Aidha Chalamila amempongeza Kamishina jenerali
Kutoka mamlaka ya udhibiti wa madawa ya kulevya (DCEA ) Aretas Lyimo kwa kufanya oparesheni kubwa mkoani humo na kukamata madawa hayo ambayo yalikuwa yanaenda kutumika na wahalifu.
Naye Kamishina Jenerali Aretas Lyimo kutoka Mamlaka ya udhibiti wa dawa za kulevya amewataka viongozi wa dini nchini katika kuweza kushirikiana katika kutokomeza Janga hilo ambalo limekua kero mkoani humo na matumizi holela kwa watumiaji wa madawa hayo.
"Ukamataji mkubwa wa madawa hayo unaenda kupunguza matumizi ya dawa hizo katika kwenda kuondoa na kutokomeza kwa janga hilo nchini hususani mkoa wa Dar es salaam. Amesema Kamishina Jenerali Lyimo.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es saalam Jumanne Murilo amesema mara kadhaaa katika kukamata wahalifu hutokana na makosa ambayo hutokana na matumizi ya dawa hizo za kulevya hivyo na kwenda kupelekea matukio mbalimbali yakiwemo Ubakaji, Wizi, na Mauaji.
Kwa kushirikiana na Mamlaka hiyo Murilo amesema watahakikisha wanavunja vijiwe vyote maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya ufukweni ambapo vinaenda kuleta Uhalifu nchini.
" sisi kama makamanda wa polisi kutoka Dar es salam Hatutokubali Usaliti katika kupunguza suala hilo kwani yeyote ambaye atahusika katika uchochezi wa matumizi hayo ya dawa haitomuacha salama sheria itachukuliwa na kufanyiwa kazi kwa wakati sahihi.
0 Comments