Na: Sheila Ahmadi
Shirika la reli Tanzania TRC limepokea vichwa vitatu vya Treni ya umeme ambavyo vimeundwa na kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa mapya 27 ya kubeba abiria huku kampuni ya Sung shin Rolling stock Technology (SSRST) imeleta mabehewa hayo na vichwa vitatu kutoka nchini Korea Kusini huku serikali imefanya manunuzi ya vichwa vipya 17 na mabehewa mapya 59.
Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika.la reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya masanja mara baada ya kupokelewa kwa vichwa hivyo 3 na mabehewa 27 ya abiria amesema mpaka sasa shirika limeweza kupokea vichwa vya treni ya umeme vinne kati ya 17 kutoka kwenye kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa 56 kati ya 59 kutoka nchini korea kusini.
Mabehewa matatu Ambayo yamesalia yanatarajiwa kuwasili nchini Mwezi Februari 2024 huku ikiwa vichwa 13 ambavyo vimebaki vinatarajiwa kuwasilli kwa awamu mbalimbali vichwa sita vitawasili mwezi machi huku vichwa saba vitawasili Mwezi April 2024.
Aidha Mhandisi masanja amesema vichwa ambavyo vimepokelewa kiutendaji vina uwezo wa Mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa huku mabehewa 27 yakiwemo kwenye madaraja ya uchumi na Biashara daraja la biashara (Bussines class) ni mabehewa 13 ikiwa kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria 45 na mabehewa ya daraja la uchumi (Economy class) ni 14 kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria 78 kwa kuzingatia viwango vya kimataifa ili kuweza kumuwezesha abiria kusafiri kwa Amani na usalama."Amesema Mhandisi Masanja"
"Shirika hilo la reli Tanzania TRC linaendelea kupokea kwa awamu vitendea kazi kea ajili ya uendeshaji wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) na zoezi la majaribio hayo ya vitendea kazi linaendelea kwa mujibu wa Mkataba ili kuhakikisha vinaendana na mifumo ya miundombinu ambayo imejengwa nchini kabla ya kuanza uendeshaji wa kibiashara.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bandari ya Dar es salaam Mrisho selemani amesema kazi ya kuhudumia bandari ni kazi yetu hivyo suala la upokeaji wa vichwa na mabehewa hayo limeenda kwa ufanisi mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi na kushirikiana na shirika la reli Tanzania TRC ili kuleta Huduma nzuri kwa wakati kwa abiria ambao wanatumia usafiri huo wa Treni.
" Sisi kama watumishi wa bandari tumeweza kusimamia na kuhakikisha usalama wa vifaaa hivyo pasipo na kutokea Ajali yeyote katika mapokezi ambayo yameanza kufanyika na hivi karibuni tunahitimisha zoezi hilo la mapokezi ya vifaa hivyo huku serikali ikiunga mkono kwenye suala hilo la kupokea mabehewa na vichwa hivyo vya Treni. "Amesema mkurugenzi Mrisho."
0 Comments