RAISI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa Mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Elimu ya Juu(HESLB) ambayo yanatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yanatafanyika tarehe Februari 17 mwaka huu.
Sambamba na hayo kabla ya maadhimisho hayo siku ya Februari 15 yatafanyika matembezi ya hisani katika viwanja vya farasi jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni rasmi anatarajia kuwa Raisi wa Mapinduzi wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Lengo la maadhimisho hayo ni kusheherekea mafanikio yaliyopatikana ndani ya Bodi ambapo idadi ya watu 8,30000 wamenufaika. Vile vile kujadili namna ya wengine kunufaika na mikopo hiyo,”alisema
Alirejea na kusema kuwa mbio za hisani zitahusisha kilometa 5,10,21.

0 Comments